Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mbunge azimiwa kipaza sauti baada ya kuhubiri siasa kanisani

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, Arusha
ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, alijikuta katika wakati mgumu wakati alipozimiwa kipaza sauti kanisani, baada ya waumini kukerwa na kitendo chake kutumia muda mwingi kuhubiri siasa na kujikosha.
Mdeye ambae aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri katika mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Rais Kikwete, alionja machungu hayo katika uzinduzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), usharika wa Sekei wilayani Arumeru, ambapo ujenzi wake uligharimu shilingi milioni 400.
Katika hotuba yake, Medeye aliwahimiza waumini hao kuchangua kiongozi anayefaa na sio chama, kwa kuangalia uwezo na utendaji wake wa kazi, huku akiwasihi Wachungaji kuombea uchaguzi ujao uwe huru na amani.
''Wananchi waangalie mtu kwanza, chama baadae, shida ya siku moja itawagharimu katika kipindi cha miaka mitano, tumieni fursa ya katiba kupata kiongozi mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo kama mimi na si mwingine,''alisema.
Medeye ambaye ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, alionya wananchi kutokubali kuhongwa kwa fedha ama kurubuniwa kwa kitu chochote, huku akiwasihi Wachungaji wafanye mahubiri yatakayowahamasisha watu wasiuze ardhi zao ovyo bali watafute wawekezaji.
Pia alipinga hatua ya yeye kuhusishwa na ukabila bali alisema anapinga ukabila kwa kuwataka wananchi kutobaguana kwa misingi dini na itikadi huku akitolea mfano mke wake anayetokea mkoani Kilimanjaro (Marangu) akihoji je amfukuze kwa kuwa yeye si Mwarusha ama Mmasai, kabila atokalo yeye.
Kauli hiyo ilianza kuibua minong'ono kwa waumini waliokuwepo ndani na nje ya kanisa, huku wangine wakisema kwa chini aondoke.
Hali hiyo ililazimu kamati iliyokuwa ikiratibu shughuli za uzinduzi wa kanisa hilo kuitana pembeni kwa muda na mmoja wapo alitoa wazo la kwenda kuzima kipaza sauti kwa muda wa takribani dakika 3, hali iliyomfanya Mbunge huyo kuamua kuondoka.

Akihutubia wadau mbalimbali katika harambee ya kuchangia fedha za hospitali ya kijiji cha Kivulul kata ya Olturoto jimbo la Arumeru Magharibi, iliyofanyika hoteli ya Golden Rose jijini hapa, Medeye alijichanganya na kujiita Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati mshereheshaji alipowaita wadau wamshike mkono.
Alitumia muda mwingi kujisafisha kwa kusema Rais anatambua mchango wake na hivyo hataacha kutatua matatizo ya wananchi.
Medeye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi wa kuachishwa kazi kama Naibu Waziri ambapo alisema watu wasihoji kuachishwa kwake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>