Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi yatuma wapelelezi kumsaka muuaji Tarime

$
0
0
Na PascalBuyaga, Tarime
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Arnest Mangu, ametuma timu ya wapelelezi wilayani Tarime, kumsaka na kumkamata mtu anatekeleza mauaji na kisha kutokomea porini.
Mtu huyo aseiejulikana amekuwa akitumia risasi kufanya mauaji ambapo watu wanane wameshauawa katika kipindi cha siku tatu.
Mtu huyo amekuwa tishio la wakazi kwa wakazi wa wilaya hiyo hali iliyosababisha baadhi ya watu kulazimika kusitisha shughuli zao kiuchumi.
Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tarime, Marco Nega, alisema tangu Januari 27 hadi sasa hospitali hiyo imepokea watu wanane waliouawa kwa risasi.
Alisema usiku wa Januari 27 mtu anayedaiwa kufanya matukio hayo alimuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Marwa dereva wa bodaboda mkazi wa Nkende wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake.
Alisema aliendelea kupokea maiti za watu wengine saba akiwemo mwanajeshi mstaafu, Zachalia Mwita (58) tangu mauaji hayo yalipoanza Januari 26.

Katika matukio mengine mtu huyo anadaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu watano ambao ni Mgosi Marwa na Juma Mwita wakazi wa Mogabiri,Joseph Richard na Gastor Richard wakazi wa Rebu pamoja na mhandisi wa ujenzi Mwasi Yomani ambao kati yao wawili inadaiwa tayari wameshafariki.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo, mkazi mmoja wa Tarime, Wambura Marwa, alisema wameshutushwa na hali iliyotokea na kuviomba vyombo vya dola kuhakikisha mtu huyo anakamatwa.

 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya, SACP Justus Kamugisha, alisema jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja anaeshukiwa kuhusika na mauaji hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>