Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mwanamke anyongwa, abakwa · Mahabusu ajinyonga chooni

$
0
0
Na Rose Chapewa, MBEYA
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Upendo mkoani Mbeya Maria Mwamangu (56) ameuawa kwa kunyongwa na kisha mwili wake kutelekezwa chumbani mwake.

Kabla ya kunyongwa, mwanamke huyo aliharibiwa vibaya sehemu za siri kwa kubakwa na watu wasiojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala alisema tukio limetokea usiku wa kuamkia jana na mwili wa marehemu ulikutwa jana mchana.

Katika tukio jengine mahabusu aliyefahamika kwa jina la Vumi Elias (30) mkazi wa Maporomoko Tunduma,  amefariki baada ya kujinyonga akiwa rumande ya polisi wilaya ya Momba.

Kamanada Mayala, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 asubuhi katika mahabusu ya polisi ya Tunduma.
Alisema, marehemu alipoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa kituo cha afya cha Tunduma.

Alisema marehemu aliingia choo cha mahabusu majira ya saa nne za usiku na kujinyonga kwa kutumia tambara la kupigia deki.

Alisema taarifa za kujinyonga ziliripotiwa na mahabusu wenzake waliokwenda chooni kujisaidia ambao walitoa taarifa kwa  askari wa zamu.

Alisema, askari hao walikimbia kwa kasi chooni na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejinyonga ingawa bado alikuwa hajafariki.

Alisema, askari hao walimchukua marehemu akiwa  hali mbaya na kumkimbiza kituo cha afya cha Tunduma ambapo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.

Kamanda huyo, alisema marehemu alikuwa akikabiliwa na kosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu na kwamba chanzo cha kujinyonga bado kinachunguzwa, mwili wake umehifadhiwa chumba cha maiti.

Wakati huo huo, mwanamme mmoja aliyefahamika kwa jina la Innocent Ndandala, amefariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na radi wakati akichota maji ya mvua wilayani Mbeya.

Akielezea tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji cha Mpakani, Thabit Mwachura, alisema marehemu alikutwa na mauti wakati akichota maji ya mvua kwa matumizi ya nyumbani ili kumsaidia mkewe ambae ni mjamzito.

Alisema wakati radi ikipiga marehemu alikuwa ameshika simu mkononi aliyoitumia kutoa mwangaza.

"Mvua ilikuwa inanyesha, marehemu alikuwa  ameshika simu ya tochi anamuRika huku akiwa anakinga maji ya mvua, ndiyo radi ikapimpiga na akafariki papo hapo," alisema.

Alisema tukio hilo lilitokea Februali 16 mwaka huu saa 9:00 alfajiri katika eneo la majengo kijiji cha mpakani Mbarali.

Aidha alisema baada ya kutokea tukio hilo alitoa tarifa kituo kidogo cha polisi Tunduma wilaya ambapo polisi walifika wakiwa na daktari na kuthibitisha kifo chake.


Alisema baada ya taratibu za kidaktari kumalizika mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>