CHAMA cha Mapinduzi, kimesema kitaendelea kutetea msimamo wake wa mfumo wa muungano wa serikali mbili, utaofanyiwa marekebisho.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma .
Alisema katika kikao hicho ambacho kilimalizika juzi usiku wa saa 8:00 chini ya Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete, wajumbe hao waliamua kuendelea kutetea mfumo huo ambo utakuwa na marekebisho katika vifungu vilivyopendekezwa na rasimu pili ya katiba.
Alisema nyingi ya chanagmoto ziliomo ndani ya rasimu hiyo zimepatiwa majibu ambapo kwa upande wa Tanzania zilikuwa nane na Zanzibar tisa.
Alisema marekebisho waliyopendekeza yatakuwa jibu tosha kumaliza kero za muungano ziliopo sasa.
Alisema hoja za baadhi ya vya vya upinzani kudai CCM ina mpango wa kuwaburuza kwa kuwalazimisha kufuata muungano wa serikali mbili, hazina msingi kwani kila kitu kiko wazi na kinaweza kugeuka ikiwa kitazingatia nguvu ya hoja.
Alisema CCM, inawataka wajumbe wa bunge la katika kuwa wazi kujadili rasimu hiyo.
Alisema huu si wakati wa kutishana kwani kuna mambo ambayo ni muhimu na yanaweza kufanyiwa kazi na kwamba jambo la muhimu ni kujenga hoja.