Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ZAWA yaanzisha kituo cha taaluma

$
0
0
Na Madina Issa
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Abdalla Mwinyi Khamis, amesema kuanzishwa kituo cha utoaji taaluma cha Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kutawawezesha wafanyakazi kufanya kazi kwa uhakika.

Aliyasema hayo alipofungua kituo hicho kilichopo  Mtoni.
Alisema ni vyema kwa mamlaka hiyo kuendeleza jitihada zao ili kituo hicho kiweze kutoa fursa nyengine za elimu.
Aidha alisema azma ya ZAWA kuanzisha kituo hicho ni kuinua kiwango cha elimu cha  wafanyakazi wake ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Alisema azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za awamu zote ilikuwa ni kuinua hali za wananchi kwa kuwawezesha wakulima na wakwezi kushiriki katika uendeshaji wa serikali yao.
Akizungumzia suala la maji safi na salama, alisema serikali ilipitisha sera ya taifa ya maji ya mwaka 2004 ikiwa na dhamira ya kuweka misingi madhubuti ya kusaidia kuandaa mikakati ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo.

Aidha alisema dhamira hiyo pia ilienda sambamba na kuanzishwa kwa sheria namba tano ya mwaka 2006 sheria ambayo imepelekea kuanzishwa kwa chombo makhsusi cha kusimamia rasilimali za maji na usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi wote.

Hata hiyo, alisema hali ya upatikanaji wa maji safikwa wananchi inaridhisha ikilinganishwa na hapo awali ambapo zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wanaoishi mijini na asilimia 65 ya wanachi wai vijijini wananufaika moja kwa moja na huduma hiyo.

Hivyo aliwataka viongozi wa mamlaka hiyo kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu hatua mbalimbali zinachukuliwa na serikali kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama.
Hata hivyo, aliliomba ZAWA kukitunza kituo hicho na kukiendeleza zaidi ili kuhakikisha kinakuwa endelevu kwa dhamira ya kuimarisha uwezo na ufanisi wa watendaji wa mamlaka hiyo.  

Nae Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dk. Mustafa Ali Garu, akitoa taarifa ya kitaalamu alisema kuanzishwa kwa kituo hicho ni miongoni mwa jitihada za serikali na mamlaka kuwapatia elimu wafanyakazi kulingana na fani zao.

Kituo hicho cha taaluma cha Mtoni kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 5 ukiwa ni ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Makaazi Duniani (UN- Habitat) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarambapo jumla ya wafanyakazi 30 wameanza ku

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>