Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Pemba walalamikia kukosa matangazo ya televisheni

$
0
0
Asha Salim na Maryam Salim, Pemba.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Pemba, wameeleza kilio chao cha kukosa huduma ya televisheni zote kupitia king’amuzi vya ZBC, jambo ambalo linawatia hofu na kusababisha wengi wao kuogopa kununua ving’amuzi.

Wananchi hao walieleza kilio hicho kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi..

Walisema kwa sasa wamepoteza tamaa kupata matangazo ya aina yoyote kupitia runinga hali inayosababisha kushindwa kupata taarifa zinazotokea duniani.

Walisema inadhihirisha serikali haikujipanga kuingia katika mfumo wa dijitali huku wakisema wameingia hasara kununua ving’amuzi visivyo na tija.

Mmoja kati ya wananchi hao, Ramadhan Salim Khamis, alimwambia mwandishi wa habari hii kwamba alilipa shilingi 75,000 kununua king’amuzi na ada ya shilingi 8,000 kila mwezi.

Kwa upande wake, Seif Nassor Seif, aliiomba serikali kupitia taasisi husika kuandaa utaratibu maalum unaotambulika kuanzia ununuzi wa ving’amuzi hadi kulipia gharama kwa wateja ambao hawapati huduma yoyote.

Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii  na Michezo Pemba, Ali Nassor Mohammed, alikiri kuwepo kwa tatizo na kusema limesababishwa na upepo uliovuma hivi karibuni.


Hata hivyo, alisema mafundi wanaendelea na matengenezo ili wananchi wapate tena huduma. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>