Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wakulima wa pamba wamjia juu RC Geita

$
0
0
Na Kadama Malunde, Kahama.
CHAMA Cha Wakulima wa pamba nchini (TACOGA), kimemlalamikia Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula, kikimtuhumu kutumia vibaya madaraka yake aliyopewa na Rais.

Mwenyekiti wa TACOGA, Elias Zizi, alisema Mkuu huyo wa mkoa anapingana na agizo la Rais Kikwete la kuwataka wakulima kutolazimishwa kujiunga katika kilimo cha mkataba mpaka kwanza wapewe elimu ya kutosha.

Malalamiko hayo ya TACOGA yanatokana na hatua ya Mkuu wa mkoa kuagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa wawekezaji wa zao la pamba wanaofanya shughuli zao katika mkoa huo kwa madai hawajatekeleza agizo la kufunga mikataba na wakulima wa zao la pamba.

Aiwataja wawekezaji waliokamatwa na kuwekwa ndani kwa agizo la mkuu huyo wa mkoa kuwa ni mwakilishi wa kampuni ya Fresho Investment, Kampuni ya ICK Cotton Co. Ltd na Kahama Oil Mill Ltd ambao wote wanafanya shughuli zao katika mkoa huo.

Aidha alisema TACOGA wameshangazwa na hatua ya mkuu mkoa na kudai ni matumizi mabaya ya madaraka aliyopewa na kwamba suala la kilimo cha mkataba ilisitishwa kwa muda.


Alisema baada ya kujitokeza changamogo hizo wadau wote walikubaliana kusitishwa kwa muda utekelezwaji wa mpango huo mpaka pale changamoto zilizojitokeza zitakapopatiwa ufumbuzi.

Alisema kitendo cha mkuu wa mkoa kimelenga kutaka kuzishinikiza pande mbili (wanunuzi na wakulima) kujiunga na mpango huo pasipo hiari yao na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka moja kwa moja maazimio ya wadau wa sekta ya pamba.

Hata hivyo, Mkuu wa mkoa pamoja na kukiri kutoa agizo la kukamatwa kwa wawekezaji hao alikanusha sababu zilizotolewa na uongozi wa TACOGA.


Alisema wawekezaji hao walikamatwa kutokana na kitendo chao cha kukiuka utaratibu wa usambazaji wa pembejeo za kilimo katika upande wa viuatilifu ambapo walitakiwa kuvisambaza kwa wakulima kwa njia ya mkopo na siyo kuwauzia.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>