Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Maalim Seif AtakaKufanywa Utafiti kujua Chanzo cha Maradhi ya Moyo Zanzibar.

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Dk. Akiva Tamir kutoka Shrika la Save the Child's Heart la Israel huko ofisini kwake Migombani Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).



Na Khamis Haji. OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema utafiti wa kina unahitajika kufanywa ili kujua chanzo cha kuongezeka kwa maradhi ya moyo Zanzibar, ikiwemo kwa watoto wadogo, ili tatizo hilo liweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Maalim Seif amesema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Save the Child’s Heart la Israel na Kinder Life Zanzibar uliofika ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko makini na inafuatilia kwa karibuni juu ya hali ya kuongezeka kwa maradhi ya moyo, hasa kwa watoto na inachukua hatua mbali mbali kuweza kukabilina na hali hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais, amesema hadi sasa watoto wengi wamenufaika na matibabu ya maradhi ya kutokana na kuwepo mashirikiano makubwa kati ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na taasisi mbali mbali zinazohusika na matibabu ya maradhi hayo.
Hata hivyo, Makamu wa Kwanza wa Rais alimueleza Kiongozi wa ujumbe huo, Dk. Akiva Tamir kutoka Israel kuwa katika hali inayojitokeza sasa ya kuongezeka kwa kasi maradhi hayo kwa watoto wadogo kuna haja ufanywe utafiti wa kina kujua chanzo halisi.
Maalim Seif aliyapongeza mashirika hayo kutokana na misaada yao kwa watoto wenye matatizo ya moyo Zanzibar, ikiwemo kuwafanyia uchunguzi na kuwapatia matibabu nchini Israel, na ameahidi kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuyapa mashirikiano ya hali ya juu.
Hadi sasa watoto 286 wa Zanzibar wamefanyiwa uchunguzi na baadaye upasuaji wa moyo nchini Israel.
Naye, Dk. Akiva kutoka Save Child’s Heart ameahidi kuwa shirika hilo litaendelea kuwapatia matibabu watoto wa Zanzibar, ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo ya moyo.
Mbali na matibabu hayo, aliahidi Shrika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na watendaji wa afya Zanzibar, ikiwemo kuendelea kuwapatia mafunzo, ili waweze kupata utaalamu zaidi katika kazi zao za utibabu.
Dk. Akiva amesema shirika hilo linakusudia kusaidia Zanzibar katika maeneo zaidi, mbali na matibabu ya maradhi ya moyo, hatua inayolenga kuwasaidia wananchi kukabilina na mradhi yanayo wakosesha kuwa na afya njema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>