Maamkizi Ya Kiislam 'Assalaamu 'Alaykum'– Amri Na Fadhila Zake - 33 - Maamkizi Ya Peponi Fadhila za maamkizi ya Kiislamu ni kubwa mno na ndiyo yatakayokuwa maamkizi ya Peponi. Tuanze na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ((إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ)) ((هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِؤُونَ)) )) لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ)) ((سَلَامٌ قَوْلًا مِن رَّبٍّ رَّحِيم (( ((Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi)) ((Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari)) ((Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka)) (("Salaam!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mwenye kurehemu)) [Yaasiyn: 55-58]. | |||
Lu-ulu-un-Manthuwrun - Hadiyth Ya 43: Wanaopendana Kwa Ajili Ya Allaah Watakuwa Chini Ya Kivuli Chakeعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: أَيْنَ الْمُتَحَابُّونَ بِجَلاَلِي الْيَوْمَ أُظِلُّهُمْ فِي ظِلِّي يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلِّي)) مسلم Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Atasema Siku ya Qiyaamah: Wako wapi wanaopendana kwa Utukufu Wangu? Leo Nitawaweka kivulini katika kivuli Changu, Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Changu)) | |||
Kizazi Kinapotea Kwa Maisha Ya Ulaya Na MarekaniMwanachuoni Ibn Al-'Uthaymiyn anasema: "Hakuna ruhusa ya kuhama kuelekea nchi za Kikafiri isipokuwa kwa masharti matatu: Awe na elimu ya diyn itakayomzuia kupotoka, awe na msimamo wa diyn utakaomzuia kuhadaika na awe ni mwenye kulazimika kwa hilo analoendea." | |||
| |||
| |||
|
↧
Nasiha ya Ijumaa
↧