Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

DC Wete awataka madereva kusaidia kupunguza ajali

$
0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
MKUU wilaya ya Wete,  Omar Khamis Othman, ameitaka jumuiya ya madereva mkoa wa kaskazini Pemba kuwaelimisha madereva wa gari za abiria na mizigo   na wale wa vyombo vya maringi mawili pamoja  na abiria kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Alisema bado ajali nyingi za barabarani zinazotokea husababishwa na madereva na abiria kutokana na kutozielewa vyema sheria za barabarani.

Kauli hiyo aliitoa   wakati akifunga kikao cha kutathimini hali ya usafiri mkoa wa kaskazini Pemba kilichowashirikisha madereva, wamiliki wa gari za abiria, wadau wa usafiri kutoka asasi za kiraia, jeshi la polisi na watendaji kutoka Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.

Alisema ni vyema pande hizo kushirikiana pamoja kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi ili waweze kuzielewa na kuzifuata.


"Hili jambo linahitaji ushirikiano wa pande zote, iwapo kila mmoja akiwajibika kwa mujibu wa nafasi yake tunaweza kufanikisha kudhibiti ajali,” alisema.

Naye Mkuu wa Idara ya Leseni Pemba, Khamis Ali Khatib, aliwataka wadau hao kushirikiana na kitengo hicho kwa kuwafichua madereva ambao wamepata leseni za udereva lakini hawafuati taratibu.

Alisema taarifa hizo zitasaidia katika kudhibiti ongezeko na ajali ambazo zinachangiwa na baadhi ya madereva wasiozingatia sheria.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya madereva mkoa huo, Tahir Omar Rehan, aliiomba serikali ya mkoa huo kuwashirikisha watendaji wa jumuiya wakati wa kupanga gari ambazo zitashiriki katika masuala mbali mbali ya kitaifa.

Alisema ni jambo la kushangaza kuona kuna gari zinatoka mkoa wa kusini Pemba kuja kufanya kazi katika mkoa huo bila wao kujulishwa.


Kwa upande wake Ofisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mwalimu Khamis Salim, ameitaka jumuiya hiyo na jeshi la polisi kuendelea kuwaelimisha wananchi na kwamba serikali ya mkoa iko tayari kupokea ushuri ili kufanikisha kupunguza ajali za barabarani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>