Na Fatuma Kitima, DSM
WADAU wa teknolojia ya habari na mawasiliano nchini (TEKNOHAMA), walikutana jana jijini Dar es Salaam kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo juu ya matumizi na ukuaji wa teknohama nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, John Mgondo, alisema serikali imetambua uhumimu wa Tekonohama hivyo kwa mara ya kwanza mwaka huu wameamua kushirikisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi.
Alisema kuongezeka na kukua sekta hiyo kumesaidia kwa asilimia kubwa kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika jamii.
Naye Mhandisi, Upendo Haule kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL), alisema tatizo la Teknohama linakuja kutokana na utayari wa wananchi kutumia teknolojia hiyo.
Alisema kwa upande wa mijini kumekuwa na utayari katika matumizi ya tekonolojia hiyo kwa jamii tofauti na vijijini.