Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

DK. SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MATREKTA YA MAHINDRA

$
0
0

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                21 Februari, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya kutengeneza matreta ya Mahindra kutoka nchini India.
Ziara hiyo ya siku mbili humu nchini inafuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais kwa uongozi wa Kampuni hiyo wakati wa ziara yake nchini Indiaaliyoifanya hivi karibuni.
Wakati wa ziara hiyo Dk. Shein alitembelea kiwanda hicho na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa kampuni hiyo ambapo Kampuni hiyo ilikubali ombi la kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendeleza kilimo.
Katika mazungumzo hayo uongozi wa Kampuni hiyo uliahidi kutuma tumi ya wataalamu nchini kuangalia namna bora kampuni hiyo inaweza kushirikiana na serikali kuendeleza kilimo.
Katika mazungumzo yake na ujumbe huo yaliyofanyika Ikulu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliushukuru uongozi wa Kampuni ya Mahindra kwa kuitikia kwa haraka wito wake kutembelea Zanzibar kujua mahitaji ya nchi katika sekta hiyo.
“Ni siku 14 tu tangu tulipoonana tarehe 7 Februari, 2014 mjini Mumbai wakati wa ziara yangu. Kwa kasi hii nina matarajio makubwa kuwa tutaweza kufanya mabadiliko ya haraka kwa wakulima wetu” Dk Shein aliueleza ujumbe huo.
Alifafanua kuwa mwitikio huo wa haraka unadhihirisha pia utayari wa Kampuni ya Mahindra ya kufanyakazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba kwa upande wake Zanzibar imejiandaa kuona ni kwa namna gani inaweza kujenga ushirikiano wa muda mrefu na Kampuni hiyo kuimarisha sekta ya kilimo nchini.
Dk. Shein aliueleza ujumbe huo kuwa ziara yao itaona jinsi kilimo kilivyokuwa na umuhimu katika uchumi wa Zanzibar na mchango wake katika kuinua kiwango cha maisha cha wananchi wa Zanzibar.
“Tunatarajia matokeo ya ziara yenu yatafungua njia ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Mahindra kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano” Alisema Dk. Shein.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Sanjay Jadhar alieleza kuwa ziara yao hiyo ni mwitikio wa wito wa Mhe Rais aliutoa kwa Kampuni yao wakati alipoitembelea hivi karibuni.
Kwa hivyo wamekuja nchini kuangalia namna Kampuni yake inavyoweza kusaidia kuimarisha kilimo nchini na kubadili hali ya wakulima wa Zanzibar.
Alifafanua kuwa ujumbe huo wakiwa na wenyeji wao uongozi wa Wizara ya Kilimo utambelea sehemu mbalimbali Unguja na Pemba yakiwemo mashamba, karakana ya matrekta pamoja na Kituo cha Utafiti wa Kilimo.
Aliongeza kuwa baada ya ziara hiyo watakuwa na mazungumzo ya pamoja na Wizara ya Kilimo na Maliasili kuhusu walichokiona wakati wa ziara na kupanga nini la kufanya kutimiza malengo ya ziara.
Ujumbe wa Mahindra ulishirikisha pia Bwana Sandesh Parab Makamu wa Mkurugenzi Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kamapuni hiyo, Bwana G.v. Rao Meneja wa Kanda Agro Tractors and Implements na Bwana Mihid Teredesai Meneja Mkuu Agro Tractors and Implements Ofisi ya Dar es Salaam.   
Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affan Othman Maalim.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles