Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi: Mabomu hayahusiani na dini ·Yalitengenezwa kienyeji ·Mmoja ya majeruhi Unguja Ukuu afariki

$
0
0
Na Mwandishi wetu
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame, amesema mabomu yaliyoripuka katika makanisa ya Mkunazini na Kijitoupele na katika mkahawa wa Mercury Forodhani, hayahusiani na masuala ya kidini, siasa wala utalii.

Aidha alisema mabomu hayo yametengenezwa kienyeji, ingawa hakuwa tayari kusema yametengenezwa kwa malighafi gani akisema ingekuwa fundisho kwa wengine kutengeneza.

Alisema sampuli za mabaki ya mabomu hayo zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna huyo alisema makachero wenye taaluma ya kisayansi kutoka makao makuu ya polisi Dar es Salaam wapo Zanzibar kushirikiana na wenzao kufanya uchunguzi zaidi.

Alisema hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, isipokuwa wanamtumia mtu mmoja ambae atasaidia kupatikana habari kuhusiana na matukio hayo.

Aliwatoa hofu wageni wanaotaka kuja Zanzibarakisema nchi ipo katika hali ya amani na usalama na jeshi la polisi litaendelea kuhakikisha amani inatawala.

Kuhusu tukio la bomu katika kijiji cha Unguja Ukuu, alisema mmoja kati ya majeruhi wanne walioripukiwa na bomu, Juma Abdallah, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Alisema marehemu akiwa na wenzake  waliojeruhiwa na bomu hilo, wakati wakiwa kwa fundi kwa ajili ya kuliyeyusha kutengeneza nanga ya mashua wakifikiria ni chuma.
Alisema majeruhi hao ambao ni wavuvi waliokota bomu hilo wakifikiria chuma na kukipeleka kwa muhunzi kwa ajili ya kutengeneza nanga.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6:00 mchana katika kijiji cha Unguja Ukuu karibu na eneo linalotumiwa na wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kwa ajili ya mafunzo.

Alisema baada ya tukio hilomajeruhi walikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja kwa matibabu na ilipofika saa 1:00 usiku mmoja kati ya majeruhi hao alifariki dunia.

Alisema tayari maiti hiyo imeshakabidhiwa kwa familia yake na kuzikwa jana kijijini kwao Unguja Ukuu.


Hata hivyo, aliwataka wananchi endapo wataokota kitu ambacho sio cha kawaida ni vyema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na kwa viongozi wa shehia ili kuepukana matatizo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>