Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi yawasaka waliohusika miripuko ya mabomu, mauaji ya polisi

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
JESHI la Polisi Zanzibar linaendelea kuwasaka watu waliohusika katika miripuko ya mabomu yaliyotokea hivi karibuni pamoja na majambazi yaliyomuua askari polisi Koplo, Mohammed Mjombo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar,Yussuf Ilembo, alisema hadi sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliekamatwa katika matukio yote mawili.

Miripuko ya  mabomu yalitokea katika makanisa mawili likiwemo la Mkunazini na mkahawa wa Mercury uliopo Malindi.
Aidha tukio la ujambazi lilitokea katika hoteli ya Pongwe Bay Resort, ambapo majambazi hayo mbali ya kumuua Koplo Mjombo pia yalimjeruhi, PC Ibrahim Juma anaeendelea kupatiwa matibabu na kumpora silaha yake aina ya  SMG ikiwa na risasi 30.

Aidha alisema bunduki iliyoporwa na majambazi hayo pia haijapatikana ingawa juhudi za kuitafuta zinaendelea.

“Hadi sasa bado hatujakamata watuhumiwa katika matukio hayo lakini tunaendelea na upelelezi,” alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya matukio ya mabomu, Kamishna wa polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, alisema mabomu yaliotumika katika matukio hayo ni ya kienyeji na upepelezi ulikuwa ukifanywa kwa kusaidiana na makachezo kutoka makao makuu ya polisi Dares Salaam.


Pia alisema miripuko hiyo ilikuwa haihusiani na masuala ya dini, siasa au shughuli za kitalii.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>