Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Watanzania waaswa kujihadhari na ugonjwa wa figo

$
0
0
Na Lorietha Laurence, MAELEZO
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, amesema asilimia 1.03 ya vifo hutokana na ugonjwa wa figo.

Alisema hayo wakati akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu siku ya afya ya figo itakayoadhimishwa Machi 13 mwaka huu mjini Dodoma.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ‘figo huzeeka, kadiri mtu anavyozeeka. Jali afya ya figo zako.’
Hivyo aliwataka Watanzania kuchukua hatadhari kujikinga na ugonjwa huo mbaya.

“Nawasihi watu wawe na taratibu za kufanya vipimo mara kwa mara, pia kujali afya zao kwa kuwekeza katika maendeleo ya afya zao ili kujikinga na ugonjwa wa figo,” alisema.

Aliongeza kuwa ugonjwa huo husababishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari na kutokufanya mazoezi mara kwa mara,msongo wa mawazo,unywaji  pombe, unene uliokidhiri,ulaji usiofaa, matumizi ya chumvi na mafuta pamoja na uvutaji sigara.


Alisema ugonjwa huo unaweza kumuathiri mtu yeyote aliye katika umri wowote, ingawa hujitokeza zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 50, ambapo takwimu zinaonesha kati ya mwanamme mmoja kati ya watano na mwanamke mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka 65 hadi 74 wana ugonjwa wa figo.

Alisema figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, husaidia kuchuja na kuondoa taka mwilini, majimaji  yaliyozidi na kudhibiti kiwango cha kemikali mwilini kwa kudhibiti shinikizo la damu.

Aliwataka  watu waepukane na ugonjwa huo kwa kufuata ushauri wa wataalamu na  kuzingatia mazoezi, kunywa  glasi 6 hadi 8 za maji kwa siku,kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zinazotokana na tumbaku, kuzingatia maelekezo ya wataalamu, kutumia dawa kwa usahihi na kufuatilia kiwango cha sukari mwilini.


Maadhimisho ya afya ya figo duniani yalianza mwaka 2006, ambapo mwaka huu yataadhimishwa kuanzia Machi 10 hadi 14 Machi, katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma, shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa huduma ya kupima afya ya figo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>