Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tanzania ina uhaba wa madaktari bingwa

$
0
0
Na Kija Elias, Moshi.
UKOSEFU wa madaktari bingwa wa ugonjwa wa figo,imekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii kupima afya zao hususani wananchi waishio maeneo ya vijijini.

Hayo yalisemwa na daktari bibwa wa figo, Francis Furia, kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili katika siku ya figo duniani ambayo ilifanyika uwanja wa Hindu Mandal mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema Tanzania ina madaktari bingwa wa figo saba pekee hali ambayo inakuwa vigumu kumfikia kila mtu, hivyo akaishauri jamii kuwa na mazoea ya kwenda hospitali kupima afya zao kabla ya ugonjwa huo haujawaathiri.

"Tuna upungufu mkubwa sana wa madaktari wa figo, hao wachache ambapo hospitali ya rufaa ya Bugando, hospitali ya rufaa ya Mbeya na hospitali ya rufaa ya Muhimbili,”alisema.

Akizungumzia kasi ya ugonjwa huo, alisema ugonjwa wa figo unasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo presha na kisukari.


Aidha aliwataka wananchi kuepuka utumiaji wa dawa pasipo kupata ushauri wa daktari, kwani dawa hizo zimekuwa zikiwaathiri watu wengi hasa kwenye figo.

"Kumekuwepo na utitiri wa dawa nyingi mitaani zikiuzwa, na wananchi wamekuwa wakizitumia bila kupima au kutafuta ushauri wa daktari na wengi wao wamekuwa wakija hospitali,  figo zao zikiwa zimeathirika,” alisema.

Kwa upande wake  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa ya KCMC, Prof.  Raimos Olomi, alisema  KCMC imejipanga kutoa huduma za afya kwa magonjwa sugu na kuongeza wataalamu wa ugonjwa wa figo.

Alisema hospitali hiyo inatarajia kuboresha huduma ya ugonjwa wa figo ambapo mwishoni mwa mwaka huu, KCMC inatarajia kupata daktari bingwa wa figo.


Naye Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dk. Ibrahim Msengi, aliwata wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya zao ili kujiandaa mapema kukabiliana na mataizo afya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>