Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi wabuni mikakati kukomesha ajali

$
0
0
Na Mohammed Mhina, DODOMA
JESHO la Polisi nchini limebuni mikakati itakayosaidia kukomesha ajali za barabarani kwa kuvishirikisha vikosikazi vya polisi jamii vilivyotawanywa katika kila kata, tarafa na shehia nchini kote.

Mikakati hiyo imetangazwa na Kamishna wa Polisi Jamii, CP Mussa Ali Mussa, wakati wa mafunzo ya maadili awamu ya pili yanayotolewa kwa askari polisi wa ngazi ya kati yanayoendelea mjini Dodoma.

Alisema mpango huo utasaidia kuwanasa madereva wazembe wasiozingatia taratibu na sheria za usalama barabarani na hivyo kupunguza ajali ziletazo vifo na majeruhi kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo wanafunzi.

Alisema vikosi kazi hivyo vinaundwa na askari polisi kutoka vitengo tofauti na kikubwa vikizingatia kazi ya msingi ya jeshi la polisi ya kuzuia na kukamata makosa mblimbali yakiwemo ya usalama barabarani.

“Kulinda usalama wa wananchi na mali zao ndio kazi kubwa ya jeshi la polisi na kwamba kwa yeyote atakayepatikana akienda kinyume na taratibu za usalama barabarani atatiwa mbaroni na hakutakua na huruma kwa mkosaji,” alisema.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Kamisheni ya Intelijensia nchini, ACP, Andrew Mwang’onda, alisema kamisheni hiyo imepanga kuwatumia Wakaguzi wa polisi  wakiwemo wakuu wa polisi wa tarafa na majimbo katika ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia kwa lengo la kubaini viashiria vya kihalifu na wahalifu.

Naye Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP, Andrew Makungu, ambaye amekokotoa idadi ya Watanzania, vitongoji, vijiji, kata, shehia, tarafa, majimbo, wilaya na mikoa iliyopo nchini ikiwemo ya kipolisi, aliwataka maafisa hao kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na wananchi katika kuwabaini wahalifu na maficho yao.


Awali Mkuu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa jeshi hilo, Naibu Kamishna, Mpinga Gyumi, alisema jeshi hilo limejipanga kuboresha mifumo ya utoaji huduma bora kwa wananchi na kujenga maadili mema ili kuepukana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>