Wawakilishi wa Zanzibar katika mkutano wa kimataifa kuhusu madawa ya kulevya huko Vienna Austria katikati ni Waziri Wa Nchi OMKR Mhe. Fatma A Ferej, kushoto ni Katibu Mkuu OMKR, Dr. Omar Shajak na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Uratibu na Udhibiti Wa Dawa za Kulevya Zanzibar ACP Kheriyangu M Khamis
Mkutano wa High Level segment wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayosimamia dawa za kulevya umemalizika Jana saa nne usiku kwa maazimio mbali mbali ikiwemo jinsi ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kudhibiti usafirishaji wa madawa ya kulevya. Miongoni mwa mikakati ya kuzisaidia nchi hizo imetakiwa UNODC kuzijengea uwezo nchi Hizo katika suala zima la upekuzi wa makontena katika milango mikuu ya nchi.
Aidha, maeneo mengine ni udhibiti wa ukulima wa mimea inayozalisha dawa za kulevya, kuweka viwango vya kimataifa cha kushughulikia matibabu ya watumiaji wa dawa za kulevya. Ama kulikuwa na mjadala
Mjadala mkubwa ambao haukuwa na maamuzi juu ya adhabu ya kifo kwa wanaoshikwa kusafirisha dawa za kulevya.
Mhe. Waziri Fatma amerejea nyumbani leo kuwahi shughuli za Bunge la Katiba wakati vikao vya watendaji na vya wataalamu vitaanza kuanzia Jumatatu 17 hadi 21 March kujadili mambo mbali ambapo Zanzibar itapata nafasi ya kuwasilisha Road Map ya mapambano ya dawa za kulevya.
Aidha. Tarehe 20 March saa 3:25 conference Room M3 tumepewa Dakika 15 kuwasilisha Uzoefu aw Zanzibar katika kushughulikia watumiaji wa dawa za kulevya na jitihada za Serikali katika mapambano.
Picha na maelezo kutoka Face book