Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Korea kumaliza tatizo la chakula Z’bar

$
0
0

 KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Misitu Ndg. Affan Othman Maalim, akitiliana Saini na Mtaalam wa Kilimo cha Umwagiliji Maji kutoka Korea,Ndg. Yoon Chang-Jin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Darajani.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Misitu Ndg. Affan Othman Maalim akibadilishana mkataba baada ya kutiliana saini na Mtaalam kutoka Korea. Ndg. Yoon Chang-Jin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Darajani.(Picha na Juma Aboud Talib - Kilimo) 

Na Khamisuu Abdallah
WIZARA ya Kilimo na Maliasili Zanzibar imetiliana saini na serikali ya Jamhuri ya KoreaKusini kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili kuimarisha uzalishaji wa mpunga nchini.

Jumla ya dola za Marekani milioni 50 zinatarajiwa kutumika katika mradi huo ambazo ni mkopo kutoka benki ya Exim ya China.

Hafla ya utiaji saini huo imefanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Darajani, ambapo kwa upande wa SMZ imewakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Affan Othman Maalim.

Akizungumza baada ya utiaji saini, mtaalamu kutoka shirika la Korea Rural Community, Dk. Yoon Chang- Jin, alisema lengo la mdari huo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na hasa mchele na kupunguza uagizaji kutoka nje.

Alisema  uzoefu wa nchi ya Koreautaweza kuisadia  Zanzibar katika sekta ya kilimo hasa miundombinu ya umwagiliaji ili iweze kuinua kilimo cha mpunga na kujitegemea kwa chakula.

Aidha mtaalamu huyo alisema mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni kupima na kuchora mabonde yote ya umwagiliaji na awamu ya pili ni kuwapelekea wakandarasi kwa  ajili ya ujenzi miundombinu ya kusambazia maji.

Alisema wameridhishwa na utafiti uliofanywa na Wizara hiyo na kuahidi kushirikiana katika uwekaji wa mazingira mazuri ya kilimo.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affan Othman Maalim, alisema mpango huo utakapokamilika jumla ya hekta 2,200 zinatarajiwa kuingizwa kwenye  mdari huo.

Aliyataja mabonde yatakayofaidika kuwa ni pamoja na Cheju, Chaani, Kibokwa na Kilombero kwa Unguja na kwa Pembani Mlemele na Makwararani.


Aidha Katibu huyo alisema mradi huo ukikamilika asilimia 50-70 ya mchele utakuwa unazalishwa Zanzibar.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>