Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

CAG kuchunguza mabilioni ya IPTL

$
0
0
Na Fatma Kitima, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Hesabu za Serikali ya Bunge (PAC), imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuafanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya Tegeta Escrow.

Aidha Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetakiwa kuanza  uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema hayo baada ya kuzungumza na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupokea maelezo kuhusu fedha shilingi bilioni 201 za akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema  Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima.
Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.

Zitto alisema  PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili taarifa ya ukaguzi huo iwe imekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.

 Alisepa pia PAC imetaka maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.
Alisema Kamati ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi shilingi  200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.

Akizungumza na waandishi wa habari, Gavana wa BoT, Prof. Benno Ndulu, alisema malipo ya fedha kutoka akaunti ya Escrow, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL zilisaini makubaliano ya kutoa fedha zilizomo katika akaunti hiyo ili zilipwe kwa IPTL.


Alisema makubaliano hayo yalijulikana kama “Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited” ambapo yaliambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na TANESCO, pamoja PS –MEM ikiwasilisha makubaliano hayo na kuiomba BoT iruhusu malipo hayo kwenda IPTL kamauhakiki ulivyobainisha.

“Kwa mujibu wa kifungu 7.7 cha makubaliano ya ufunguzi wa akaunti (Escrow Agreement) fedha zilizomo kwenye akaunti hiyo zingeendelea kuwepo na kuwa katika mamlaka ya Escrow na kwamba fedha hizo zingetolewa tu kama kuna hukumu ya mahakama inayoamuru kutolewa kwake au pande mbili za makubaliano,”alisema.

Aidha alisema Septemba 5 mwaka 2013,mahakama kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi uliogusa umiliki wa fedha zilizopo katika akaunti hiyo,iliyokuwa chini ya udhibiti wa BoT,kutokana na uamuzi  huo uliotokana na maombi yaliyofanywa na mmoja wa wanahisa wa IPTL- VIP (Engineering and Market Limited) ambaye aliomba mahakama iridhie kufutwa kwa shauri ambalo VIP walilifungulia mahakamani (Misc.Civil Application No.49/2002 na Misc.Civil Application No.254/2003.

Alibainisha kuwa maombi hayo yalitokana na makubaliano ya mauzo ya hisa za VIP katika IPTL kwenda katika kampuni ya Pan Afrika Power Solutions (T) Limited PAP.

Alisema katika uamuzi huo,mahakama pamoja na mambo mengine iliridhia kufutwa kwa mashauri na kuelekeza kwamba mali zote za IPTL,ikiwemo kiwanda cha kufua umeme zikabidhiwe kwa mmliki mpya wa IPTL ambaye ni PAP.

Hata hivyo alisema  fedha za ‘capacity charge’ ziligawanyika katika makundi mawili moja fedha za kitanzania wakati kiasi kingine ni dola za Marekani.

Alianisha makundi hayo ya fedha yalikuwa yamewekezwa katika uwekezaji wa ndani na wa nje, kwa kuzingatia kifungu 3.4 cha escrow agreement, ambapo hadi kufikia Novemba 25 mwaka 2013,salio katika dola za Marekani,pamoja na faida ilikuwa ni dola 22,198,544.60,huku salio katika fedha za kitanzania zilikuwa ni shilingi 161,389,686,585.34 ikijumuishwa na faida katika uwekezaji shilingi 5,297,550,682.04.


Alisema Julai 5 2006 serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL pamoja  na BoT, waliingia makubaliano ya kufunga akaunti maalum (escrow).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>