Na Ali Issa na Miza Othman Maelezo.
Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mfenesini Mjini Unguja wameamua kuiunga mkono kwa makusudi hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bungeni wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa Bunge maalumu la Katiba huko Dodoma.
Hayo yamesemwa leo huko Bububu Wilaya ya magharibi Mjini Unguja na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mbarouk Mrakib Mbarouk wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Vijana wa chama hicho ofisini kwake Bububu.
Amesema hutuba ya Rais kikwete ni hutuba ilio jaa hekima na busara juu ya mustakabali mzima wa muundo wa serikali waitakayo Watanzania.
Amesema kutokana na kauli za Rais huyo hakuna budi kwao kuiunga mkono kwani ndio muelekeo wao katika muundo wa serikali waitakayo wanaccm ambayo yenye umoja na mshikamano kwa watanzania.
Aidha amesema alihamisha kuwa kwa wale wajumbe wanaohudhuria kikao cha Bunge la Katiba huko Dodoma hawana budi kuhakikisha wanatoa maoni ya wananchi wao ikiwa ni njia moja ya kuwafanya wananchi hao kuleta umoja na mshikamano katika Taifa lao.
Mwenyekiti huyo alimpongeza kwa dhati dkt. Kikwete kwa kulizungumzia suala la mipaka ya Tanzania, mito, maziwa,na bahari ambalo lilisahauliwa ndani ya katiba hiyo.
Pia alimshukuru Rais huyo kwa kuyazingatia masuala ya Zanzibar juu ya kujiunga na nchi za visiwa duniani ,umoja wa kiislamu OIC, na suala la mafuta na gesi asilia.
Mwenyekiti huyo aliwakumbusha wabunge wa Bunge maalumu wa CCM kuijadili katiba hiyo kwa kina ili lengo la kuwepo kwao bungeni ni kufanikiwa kwa katiba wanayo itaka wanaCCM.