Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ni Zanzibar au ni Unguja?

$
0
0

Ninapata taabu kuamini kwamba waandishi wengi  na wanataaluma ya habari wanashindwa kutumia matumizi sahihi ya visiwa vya Unguja, Pemba na Zanzibar.

Utaona wakati mwengine mwandishi anatumia jina la Zanzibar akimaanisha Unguja,wakati mwengine hutakiwa kutumika jina la Pemba lakini litatumika la Zanzibar. Ingawa kimaana huweza kuwa ni sawa lakini kimatumizi inawezekana kuwa na makosa

Tatizo hili nimeliona kwa waandishi wengi wa nyumbani, wa kigeni na kutoka upande wa pili wa Muungano wakijikuta wakiingia katika mtego huu.
Sehemu ambayo huwa nasikia kutajwa kama ni Unguja au Pemba ni pale panapotajwa mikoa ya Kusini/Kaskazini kama ni Unguja au Pemba na wilaya zake.

Mkanganyiko huu, kwa uoni wangu mdogo, umepelekea kwa kiasi kikubwa  kufa kidogo kidogo kwa jina la Unguja na badala yake kutumika Zanzibar kama ni Unguja  na ukiangalia kwa jicho pevu itapelekea uonevu tutakaowafanyia wana wa Kizanzibari ambao hujulikana hivyo kwa sababu ya kutoka katika Visiwa viwili vikuu vya Pemba na Unguja.

Tutafute njia muwafaka ya kutumika kwa majina haya mawili bila ya kuathiri jengine katika matumizi na mafhuum (maana) yake pia kabla ya kulipoteza jina la asili la Unguja kama hatujaanza sasa.

Na Mdau anaelienzi jina la Unguja

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>