Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Uingereza yaja na utaratibu mpya mfumo wa viza

$
0
0
Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania umesema unakusudia kufanya mabadiliko ya utaratibu wa maombi na utoaji viza kwa Watanzania wanaotaka kwenda nchini Uingereza kwa kufungua ofisi zitakazokuwa zinatoa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.
 
Hapa ndipo zilipo ofisi za ubalozi wa Uingereza jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Shughuli za viza zitahama kutoka jengo hili na kuhamia katika eneo tofauti jijini.
Mkurugenzi wa masuala ya viza ya Uingereza kwa nchi za Afrika Bw. Kashif Chaudry, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema pia wanakusudia kuanza kulipia huduma hiyo kwa njia ya simu za mkononi.
Chaudry amesema kupitia utaratibu huo mpya, maombi yote ya viza sasa yatakuwa yanafanyika nje ya jengo la ubalozi na kutaja eneo moja jijini Dar es Salaam kuwa ndiko ambako watu wanaweza kuomba na kupata viza za kuingia nchini Uingereza.
Amelitaja maeneo hayo kuwa ni katika jengo la Viva Towers lililopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza usumbufu kwa watu wanaoomba kibali cha kuingia Uingereza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>