Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Stella Vuzo akitoa ujumbe wa siku ya Kimataifa ya kumbukumbu ya wahanga wa Utumwa na Biashara ya Utumwa ngambo ya Bahari ya Atlantiki kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern (hawapo pichani) walipotembelea maeneo yaliyokuwa yakiendesha Biashara ya Utumwa Zanzibar.
Mtembezaji wageni Peter Mashauri wa Kanisa la Mkunazini akiwapa maelezo wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Ubungo Modern ya Dar es salaam walipotembelea maeneo ya Kihistoria yaliyokuwa yakiendesha Biashara ya Utumwa Zanzibar katika siku ya Kimatafa ya kumbukumbu hiyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi, 25 .
Wanafunzi wa Sekondari ya Ubungo wakimsikiliza mtembezaji wageni (hayupo pichani) wakiwa katika chumba kidogo kilichokuwa kikihifadhiwa watumwa waliokuwa wakisubiri kusafirishwa kwa ajili ya kupigwa mnada katika Kanisa Kuu la Mkunazini.
Wanafunzi wa Ubungo Modern wakiangalia vitabu vya Historia ya Zanzibar walipotembelea Kasri ya Wananchi Forodhani Mjini Zanzibar
Wanafunzi wa Ubungu wakipata maelezo kutoka kwa mtembezaji wageni Peter Mashauri wa Kanisa la Mkunazini walipotembelea magofu ya kuhifadhia watumwa yaliopo Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanafunzi wa Ubungo wakiangalia sehemu waliyokuwa wakihifadhiwa watumwa katika maeneo ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanafunzi wakiangalia Bandari ndogo iliyokuwa ikitumika kupokelea na kusafirisha watumwa katika maeneo ya Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja.
(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.)