Mratibu wa mafunzo juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru (NTBs) Aboud Hassan Serenge akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya siku tatu kwa washiriki wa mafunzo hayo yanayofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa TradeMark Afrika Mashariki kupitia Tanzania Asaac Mtwale akizungumza na washiriki wa mafunzo juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru katika Hoteli ya Grand Palace Malindi (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Julian Rafael.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Julian Rafael akifungua mafunzo ya siku tatu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Julian Rafael (hayupo pichan) katika Hoteli ya Grand Palace Malindi.
(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.)