Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mnazimmoja yakana kuzembea

$
0
0
Na Madina Issa
UONGOZI wa hospitali kuu ya Mnazimmoja umeelezea kusikitishwa na tukio la mtoto  Mwanaidi Shukuru Mustafa (0.2) ambae amekatwa mkono, wakati akipatiwa matibabu.

Tukio hilo limetokeea kutokana na tatizo la ‘gagril’ ambalo sio la makusudi inavyodaiwa na watu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, daktari kutoka kitengo cha watoto katika hospitali hiyo, Farhat Salum, alisema tatizo hilo limesababishwa na damu kutozunguka katika mkono wake.

Alisema baada ya kuwekewa ‘kenyula’ katika mkono wake kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya kifua cha nimonia,mkono wake ulikuwa unavimba.

Aidha alisema baada ya kuona tatizo hilolinaendelea muuguzi wa zamu alitoa taarifa kwa daktari kumuangalia kwa ajili ya kupatia matibabu zaidi na kujua tatizo lake.

Alisema baada ya daktari kufika alimwangalia na kugundua kuwa damu yake haitembei na kumuita daktari wa upasuaji ili amuangalia zaidi na kushauri mkono ukatwe ili tatizo lisiendelee kumuathiri.

“Kwa kweli sio uzembe wa muuguzi wala daktari wa zamu bali ni tatizo la kiitaalamu ambalo linaweza kumtokezea mtu yeyote na huyu mtoto limemtokezea wakati alipotiwa ‘kenyula’ kwa ajili ya kuchomwa sindano matokezea yake limekuja tatizo hilo,” alisema.

Aidha lisema baada ya kupata taarifa hizo uongozi wa hospitali ulikaa pamoja na muuguzi na daktari wa zamu wa siku hiyo na kulizungumzia tatizo hilo lakini waligundua hilo ni tatizo la ‘gagril’.


Mbali na hayo ameishauri jamii kuondoa dhana ya kuwepo uzembe wa muuguizi na daktari dhidi ya matatizo yaliyomkumba mtoto huyo.

Hata hivyo, alisema hali ya mtoto inaendelea vizuri na ugonjwa wa nimonia unaomsumbua unaendelea kupatiwa matibabu na mkono wake unaendelea vizuri.

Mapema mama mzazi wa mtoto huyo, Khadija Abdallah Salum, alisema mtoto wake alikuwa nasumbuliwa na kifua cha nimonia na alipofika hospitalini aliandikiwa sindano.

Alisema baadae mtoto wake alitiwa kenyula kwa ajili ya kuchomwa sindano lakini daadae mkono ulianza kuvimba.

Alisema baada ya kuona tatizo hilo alimuita muuguzi, lakini alimjibu kwamba  mtu huanza kufa kuanzia miguu seuze huyo mwanao huku akimwangalia mkono wake.

Alisema baadae alimwita daktari kuja kumuangalia zaidi na kugundua kuwa mwanawe ana tatizo na kumpeleka ICU na kukaa siku tano huku madaktari wakienda  kumwangalia na siku ya Jumatatu walimwambia kuwa mkono wa mwanawe haufai na utolewe ili sumu isienee zaidi.

Alisema hivi sasa anaandikiwa dawa hizi na hizi na pesa hana na baada ya siku hubadilishiwa dawa na kuambiwa hivi sasa usimpe hizi.

Ameiomba serikali kumuangalia kwa jicho la huruma kwani yeye ni mnyonge na hana uwezo wa kumuhudumia mtoto wake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>