Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akitoa huduma za vyakula katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pamoja na watendaji wa Wizara yake hapo Nyumbani kwake Mazizini.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiwa katika futari ya pamoja Nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wa ofisi yake mara baada ya futari ya pamoja kati yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Familia yake
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha zake mara baada ya futari ya pamoja na watendaji wake hapo nyumbani kwake mazizini.
Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar na watendaji wa taasisi nyengine za Serikali na wakaazi jirani ya nyumba ya Balozi Seif wakipata futari ya pamoja nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Picha na Hassan Issa wa - OMPR – ZNZ.
NaOthman Khamis Ame, OMKR
Watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wanapaswa kuendeleza tabia waliyokuwa nayo ya kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ili kufanikisha lengo lililokusudiwa na Taifa.
Nasaha hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufutari pamoja na baadhi ya Wafanyakazi hao hapo nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Futari hiyo pia iliwajumuisha majirani wa Balozi Seif waliyozunguuka makazi yake, Kamati ya wananchi wanaoishi katika eneo la Uwanja wa ndege pamoja na baadhi ya Wawakilishi na watendaji wa Taasisi nyengine za Serikali.
Alieleza kwamba wafanyakazi mara nyingi wanakuwa kazini pamoja kwa kipindi mrefu katika harakati za za kimaisha za kila siku jambo ambalo wanastahiki kupendana na kushirikiana kwa vile wanaishi kama familia moja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wafanyakazi hao wa Ofisi yake kwa kazi kubwa ya kuandaa bajeti ya Wizara hiyo na hatimae kupitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Kikao cha kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara za Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2013 /2014.
Akizungumzia funga ya mwezi mtukufu wa ramadhani inayoendelea Balozi Seif aliwataka waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wafanyakazi hao kutekeleza ipasavyo ibada hiyo katika taratibu zilizivyowekwa na Dini.
Alisema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umekuwa kigezo kikubwa kwa waumini wa Dini ya Kiislamu ambao huwafundisha mambo mengi endapo watayaendeleza yatawajengea hatma yao njema ya baadae.
Mapema wakitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wa Ofisi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Khalid Salum Mohd wamemshukuru Balozi Seif kwa utaratibu wake wa kuwashirikisha watendaji wake katika futari ya pamoja.
Walisema tabia hiyo kwa kiasi kukubwa imekuwa ikiendelea kuongeza upendo baina ya Viongozi na Wafanyakazi hao sambamba na wale wananchi wanaowahudumia.
“ Hii ni tabia ya upendo kati ya Uongozi na wale wanaowaongoza ambayo hujenga udugu na ushirikiano unaoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao “. Alifafanua Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid.