Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hawana maji tokea uhuru

$
0
0
NaJumbe Ismailly,IRAMBA
PAMOJA na kukamilika miundombinu ya maji tangu mwaka 1998, zaidi ya wakazi 1000 wanaoishi katika kaya 335 zilizopo     kijiji cha Meli,tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba,mkoani Singida,hawana huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.

Hayo yamebainishwa na wananchi wa kijiji hicho kufuatia uchunguzi uliofanywa na shirika moja lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na uboreshaji wa afya la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mkoani Singida kutaka kufahamu sababu za wananchi hao kutokuwa na huduma hiyo.

Wakizungumza kwa jazba na kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema tangu mwaka 1978 tanki la maji pamoja na miundombinu ya maji ilipokamilika kujengwa, Idara ya maji wilaya,imeshindwa kupeleka mashine ya kusukuma maji iliyokuwepo kwa kile ilichodai imeibiwa.

Baadhi ya wananchi hao, Shiguna Shiguna,ambaye pia ni Ofisa kilimo na maendeleo ya mifugo wa kijiji cha Meli, alismea  wananchi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maji tangu walipopata uhuru.


Kwa mujibu wa mtumishi huyo wa serikali pamoja na kuwepo wakuu wa idara ya maji na kuhudhuria mikutano ya kijiji,walikuwa wakitoa majibu ya kuwa wapo njiani na haijafahamika mpaka sasa ni njia ipi waliyopitia.

Naye mmoja wa wajumbe wa nyumba kumi katika kijiji hicho,Maria Kitundu, aliyeonekana kuguswa zaidi ya tatizo hilo, alisema kutokana na tatizo hilowamekuwa wakilazimika kutoka saa 11:00 alfajiri kwenda kutafuta maji.

Hata hivyo, mwanamama huyo aliweka bayana kwamba pamoja na kutoka usiku lakini waume zao hawajali umbali uliopo na uchache wa maji hivyo wanapochelewa kurudi nyumbani hufuatwa na waume zao na kupigwa.

Naye John Pyuza, alisema licha ya kijiji kufungua akaunti ya maji baada ya viongozi kutoka wilayani kufika kijijini hapo na kuwahamasisha juu ya kuwapelekea huduma hiyo, bado maji yameshindikana.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HAPA mkoani Singida, David Mkanje, alisema kupitia shirika la World Vision Tanzania linalofadhili mradi huo,katika wilaya za Singida vijijini na Iramba mkoani Singida na Nzega,mkoani Tabora zilizopo katika mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii (SAM),kati ya shilingi bilioni 30 zilizotengwa kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji safi na salama katika wilaya hizo, shilingi bilioni 23 zimeshatumika na kwamba mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba.


Akizungumzia hoja ya wananchi,Mhandisi wa maji wa wilaya ya Iramba, Eng.Leonidas Rweyemamu, alisema licha ya kutoikubali taarifa ya shirika hilo pamoja na malalamiko ya wananchi,alisema taarifa zilizotolewa hazina ukweli wowote. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>