Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Tanzania na Japan zimesaini mkataba wa shilingi bilioni 6.02 kwa ajili ya kununua mbolea ikiwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Servacius Likwelile.
Alisema msaada huo utawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa chakula hasa kwa wakulima pamoja na kuwainua kiuchumi.
Alisema pamoja na kuinua kiwango cha mkulima wa chini pia kuwekeza katika miundombinu hasa masoko ili kuinua sekta ya kilimo nchini.
Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaki Okada, alisema wameamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuinua sekta ya kilimo Tanzania .
Alisema lengo ni kununua mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dk.Yamungu Kayandabila, aliishukuru Japan kwa msaada huo muhimu.