Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Uwanja wa mapembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) wakati alipotoa maelezo ya ramani ya kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho leo,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali maalim Abdalla Mzee
wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,(kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,na (kushoto) Katibu Mkuu Bi Mwanaidi Saleh,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,(kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,na (kushoto) Katibu Mkuu Bi Mwanaidi Saleh,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Na Ali Issa-Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameagiza kufanyika mazungumzo kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na Wizara ya Ardhi,Makaazi Maji na Nishati ili kupatikana Hati miliki katika eneo la Ujenzi wa Mnara wa Mapinduzi katika eneo la Michezani Mjini Zanzibar.
Hayo ameyasema leo alipofanya ziara maalum kuangalia hatua ya ujenzi wa Mnara huo na Kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo unaosimamiwa na Mfuko huo.
Amesema kupatiwa hati miliki ya eneo la Michezani ni suala la kukaa pamoja taasisi hizo husika kwani eneo hilo linamilikiwa na Serikali na sio la mtu binafsi.
“Nendeni mkazungumze na watu wa Ardhi mkubaliane halafu nijue mulipofikia haya yote ni maeneo ya Serikali,”alisema Dkt. Shein.
Alisisitiza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuliendeleza eneo hilo la Michezani kwa kujenga Mnara utakao kuwa na Maduka na Mikahawa hivyo kuna haja kukaa na wafanya biashara wa eneo hilo kufanya mazungumzo na kuwatafutia maeneo mengine ya kuendeleza biashara zao.
“Wafanya biashara wanapenda maeneo mazuri, sidhani kama watakataa kupatiwa sehemu nyengine ili kuendeleza biashara zao,”aliongeza Rais wa Zanzibar.
Aidha Dkt. Shein alifurahishwa na hatua iliofikiwa katika ujenzi wa majengo hayo na kusema kiwanja cha Kariakoo kinapaswa kuwa cha kisasa na bora kwani kitatoa huduma nyingi za kibiashara kitakapo malizika.
Hata hivyo alisema kiwanja cha Kariakoo kimezungukwa na majirani hivyo upo umuhimu kukaa na majirani hao kwa mazungumzo ili kupatikana usalama wa eneo hilo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Abdulwakil Haji Hafidh alisema kuwa kiwanja cha Kariakoo hadi sasa kimeshagharimu shilingi bilioni 10 na mpaka kitakapomalizika kitagharimu shilingi bilioni 13.5 za Tanzania.
Alisema kiwanja hicho kinatarajiwa kutoa huduma kuanzia mwakani kwani hatua kubwa ya ujenzi imekamilika na vifaa vingi vimeshawasili na vinasubiri kufungwa.
Abdulwakili alisema kuwa kiwanja hicho kitakuwa na huduma zote muhimu kwa binaadamu ikiwemo maduka, mikahawa na maeneo ya kupambia maharusi na burudani nyengine.
Aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanja hicho utakapo kamilika wataunda bodi maalu itakayojitegemea kukiendesha.
Wakati huo huo Dkt. Ali Mohamed Shein alitembelea eneo la Skuli ya Sekondari ya Lumumba na kukemea tabia ya kuvamia eneo hilo kwa kuchimbwa mchanga na kuligeuza kuwa gereji.
Amesema Serikali inampango wa kulizungushia uzio na matayarisho yake yamekamilika na karibuni tenda ya ujenzi itatangazwa ili kuirejeshea skuli hiyo hadhi yake ya zamani.