Na Haji Nassor, PEMBA
WAKULIMA wanaojishughulisha na kilimo cha tungule na mahindi, shehia ya Mjini ole wilaya ya wete Pemba, wameiomba Serikali kuwapatia pembejeo za kilimo hicho, ili kiweza kuleta maendeleo ya kiuchumi na na kukuza pato lao.
Walisema wamekuwa wamekuwa wakijishughulisha na kilimo hicho, bila ya kuwa na pembejeo za uhakika, jambo ambalo husababisha kwa baadhi ya wakati kupata mavuno duni.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kijijini kwao wakulima hao alisema, ni jambo la busara kwa Serikali kuangalia kilio chao hicho ili na wao wapate mafanikio.
Mmoja kati ya wakulima hao, Aisha Salim Hemed, alisema kilimo hicho ndicho ambacho huwapatia pato na kuendesha maisha yao, ingawa hawajapatiwa msaada wowote hasa wa pembejeo.
‘’Sisi tunaendesha kilimo hichi lakini hatujawahi kupata pembeo kama vile mbolea na mbegu za kisasa’’,alifafanua mkulima huyo.
Nae Maryam Omar Idrisa alisema kuwa, hadi sasa wamekuwa wako nyuma katika maendeleo ya kilimo, jamba ambalo huwakatisha tamaa katika shughuli hizo na kutojipatia tija yoyote katika sekta hiyo.
Aidha alieleza kuwa wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika shughuli zao ikiwa pamoja na kutokuwa na maeneo ya kutosha ya kulimia.
Hata hivyo alifahamisha kuwa katika shughuli zao hizo za kilimo wamekuwa wakikosa huduma muhimu ya kupatiwa madawa katika mashamba yao kutokuwa na wataalamu wa kilimo (bwana shamba).
‘’Sisi wenyewe tunajilimia tu tunavyojua hatupati taaluma kutoka kokote kule wala kupatiwa madawa kwa ajili ya kilimo chetu tunajitegemea wenyewe kila kitu’’, alisema.
Kwa upande wake, Maryam Said Ali aliiomba Serikali kuwapatia mitaji ya kuwawezesha wao wakina mama iliwaweze kujikombao na umasikani na kuweza kuwapatia watoto wao huduma zilizo bora kwa maendeleo ya Taifa.
Alisema kuwa iwapo Serikali ikiwapa mtaji huo kwa ajili ya maendeleo yao basi itawasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuweza kujikomboa na umasikini.