Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Bunge Maalum la Katiba Kuendelea na Kikao Chake Leo Dodoma.

$
0
0
Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Bunge maalum la Katiba, wanarejea leo baada ya mapumziko ya karibu wiki moja ya kuandika ripoti.

Mkutano wa leo, utatoa nafasi kwa Wenyeviti wa Kamati 12 kuanza kuwasilisha ripoti zao baada ya kupitia kipindi kigumu cha  mijadala na mivutano ndani ya kamati.

Ripoti zitakazowasilishwa zinahusu sura ya kwanza na ya sita, ambazo zinagusa moja moja hatma ya Muungano.

Wadadisi wa mambo wanasema sura hizo zitazua mjadala mpana na mkali miongoni mwa wajume wanaounga mkono muungano wa serikali tatu na wale wanaounga mkono muungano wa serikali mbili.

Akizungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bunge la katiba, Samuel Sitta, aliwaasa wajumbe kujadili na kuchambua kwa kina sura hizo kwa sababu ndio zinazogusa uhai wa Muungano.


Muungano wa wajumbe wa katiba ya wananchi (UKAWA) wanashikilia msimamo wa muungano wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu huku muungano wa wajumbe wa katiba ya Watanzania, wakisisitiza serikali mbili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>