Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Amour, akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Ndg. Abrahaman Mwinyimbegu na Mjumbe wa Bodi na Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamiii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Abdulwakili Hafidh, wakiingia katika ukumbi wa hafla hiyo Zanzibar Beach Resort Mazizini jana usiku.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, Ndg. Abrahaman Mwinyimbegu, akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Mstaafu wa PBZ Ndg Ame Haji Makame kwa kumaliza muda wa Utumishi katika PBZ baada ya kutumikia PBZ kwa muda wa miaka 40. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini, Zanzibar jana usiku 14-4-2014.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd. (PBZ) Ndg. Juma Amour, akizungumza machache katika hafla hiyo ya kumuaga aliyekuwa Msaidizi Maalum wa Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Ame Haji Makame, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Afisa Rasilimali Watu wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Rajab Abdallah,akisoma wasifu wa Afisa Mstaaf wa PBZ Ndg.Ame Haji Makame, wakati wa hafla alioandaliwa na Uongozi wa PBZ kwa ushirikiano wake wakati wa Akiwa Mfanyakazi wa Benki, Ndg Ame Haji Makame ameshika nyadhifa mbali katika Benki hiyo kuazia ngazi ya chini hadi kufikia Afisa Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji, ameitumikia PBZ kwa muda wa miaka 40.
Aliyekuwa Msaidizi Maalum wa Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Ndg. Ame Haji Makame akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga kwa utumishi wake wa muda mrefu katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa muda wa miaka 40, na kutowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa PBZ, na kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao na kujiwekea ufanisi katika kazi zao za kila siku.Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Maofisa wa PBZ wakimsikiliza Mstaaf wa PBZ Ndg. Ame Haji Makame, akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kumuaga iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mjumbe wa Bodi ya PBZ akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ wakati Mwenyekiti wa Bodi akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga Ndg. Ame Haji Makame.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, (PBZ) Ndg. Abrahaman Mwinyimbegu, kushoto akimkabidhi Seti ya Masofa aliyekuwa Msaidi Maalum wa Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Ame Haji Makame, wakishuhudia makabidhiano hayo kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt Hafidh , Afisa wa PBZ,Bi Saadie na kulia Mkurugenzi Mtendakji wa PBZ Ndg. Juma Amour, makabidhiano hayo wamefanyika wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Amour akimkabidhi zawadi iliotolewa na Wafanyakazi wa PBZ kwa Ndg. Ame Haji Makame, katika tafrija la kumuaga baada ya kuitumikia Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd kwa muda wa miaka 40 ya kazi katika PBZ.
Benki ya watu wa Zanzibar PBZ imepata faida ya shilingi bilioni 7 ikiwa ni mara tatu zaidi ya faida ya makusanyo yake .
Mkurugenzi mtendaji wa PBZ Juma Amour amesema makusanyo hayo ni ya jumla bila ya kodi Na mi hatua muhimu kwa maendeleo ya banki hiyo yanayoimarika kila siku.
Akizungumza katika hafla ya kumuaga msaidizi wa Mkurugenzi Ame Haji Makame anaemaliza muda wake wa utumishi wa umma iliyowashirikisha wajumbe wa bodi na maafisa wa benki hiyo amesema mafaniko hayo yamechangiwa na utoaji huduma bora kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya PBZ amefahamisha kuwa benki hiyo inathamini mchango wa mstaafu huyo alietumika taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka 40 na aliesaidia kufikia mafaniko hayo.
Kwa upande wake Ame Haji Makame ameushukuru uogozi na wafanyakazi hao kwa ushirikiano wao na kuwataka wafanyakazi kukinai na maslahi wanayoyapata katika utendaji wa kazi zao.