Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wabunge watakiwa kujali maslahi ya umma

$
0
0
Na Khamis Haji OMKR
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewasihi wabunge wa bunge maalum wanaojadili rasimu ya pili ya katiba kuweka mbele maslahi ya nchi na kuelewa kuwa Jamhuri ya Muungano imetokana na nchi mbili zilizokuwa dola huru.

Alisema hayo wakati akifungua maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibaryanayoendelea hadi Aprili 19 katika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema wabunge hao wajielewe kuwa wana wajibu mkubwa kwa Watanzania, lakini pia wafahamu kwamba kazi yaokubwa ni kuhakikisha kero za Muungano zilizodumu kwa muda mrefu tokea Muungano huo ulipoasisiwa miaka 50 iliyopita zinakuwa historia.

“Nawasihi wabunge waangalie maslahi ya nchi mbili zilizokuwa dola huru, wafahamu kuwa ziliungana kwa hiari, lazima tusikilize hisia za kila upande na wala tusichukue maamuzi ya haraka, tukifanya hivyo  tusababishia tusipate katiba iliyo bora,”, alionya.

Alieleza ipo haja wabunge wajiulize katiba inayotafutwa itatatuaje kero zilizopo, je itakidhi haja na kukabili changamoto zilizopo, ikiwemo mgogoro wa katiba ulioelezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba, kati ya katiba ya Jamhuri na ile ya Zanzibar.

“Nadhani Warioba alipotoa mapendekezo ya Tume aliona ugumu wa suala hili, lazima hilo lizingatiwe. Watanzania wanataka Katiba ambayo italeta usawa na nchi mbili zilizoungana kuheshimiana,” alieleza.


Alisema huu si wakati wa kikundi fulani kujifanya kina haki zaidi, lazima kila upande usikilizwe unasemaje, ili baadaye maoni na mawazo tafauti yaweze kupimwa na kufanywa maamuzi sahihi ambayo yatawezesha kusaidia kupatikana  katiba itakayodumu kwa miaka mingi ijayo.

“Tujiepushe na kikundi kimoja kujifanya kina haki zaidi, sote tuna haki sawa,” alisisitiza Makamu wa Kwanza wa Rais.

Akitoa shukurani kwa mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema wabunge wa bunge maalum wanaoendelea na mjadala mjini Dodoma wako makini na watapima kila hoja inayowasilishwa ili hatimaye waweze kupata katiba iliyo bora.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge, alisema maonesho hayo ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibarni fursa ya kihistoria kwa wananchi wa Tanzania kwa vile hayajapata kufanyika kwa miaka 50.


Alisema wananchi watapata taaluma na taarifa mbalimbali zinazohusu mafaniko na matarajio ya taasisi mbali mbali za Muungano, pamoja na kupata fursa ya kutoa maoni yao juu ya mipango inayotekelezwa.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>