Baadhi ya wajumbe wanchi wafadhili na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakielekea katika ukumbi maalum uliowekwa kwa ajili ya mkutano kuzungumza na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya MwembeMakumbi wilaya ya Mjini Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Bwana Ladislaus Mwamanga akiwatambulisha baadhi ya wageni walioshiriki katika kikao cha kujifunza kutoka kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja ambako ujumbe huo umekuweko kwa siku Tatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Taifa Bwana. Ladislaus Mwamanga akiwa na Wakuu wa Benki ya Dunia wakiwasikiliza Walengwa wa Mradi wa Tasaf wa kunusuru Kaya Masikini zenye mazingira magumu, walipofika katika moja ya Shehia ziliko katika mpango huo shehia ya Muembemakumbi Wilaya ya Mjini Unguja.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bwana Amedius Kamagenge akitoa ufafanuzi wa moja ya masuala yaliyojitokeza katika kikao cha pamoja kati ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja na wadau wa maendeleo ambao wamefanya ziara ya kutembelea shehia ya muembemakumbi ikiwa ni moja ya shehia iliobahatika na mradi huo wa Tasaf Awamu ya Tatu.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi wafadhili waliohudhuria kikao cha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi wilaya ya Mjini Unguja wakisikiliza maoni kutoka kwa walengwa wa mpango huo (hawapo pichani) Nyuma ni Meneja wa Fedha wa TASAF Bwana Nyamuko na Meneja Ukaguzi wa TASAF Bwana Mziray wakifuatilia mjadala huo.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kusimamia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Shehia ya Mwembemakumbi ,wilaya ya Mjini Unguja akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoibuliwa na baadhi ya wajumbe kutoka nchi wafadhili wa mpango huo juu ya namna walengwa wa mpango huo walivyopatikana.na kufaidika na mpango huo
Mdau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, akihoji walengwa jinsi ya mafanikio walioyapata katika mradi huu wa TASAF wa kunusuru Kaya zenye mazingira magumu, kushindwa kuwahudumia watoto kwenda skuli na kupata matibabu. kupitia mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini katika shehia ya Mwembemakumbi ,wilaya ya Mjini Unguja akitoa mawazo yake juu ya namna Mpango huo unavyomunufaisha.na kuboreshwa ili kuweza kuwanufaisha wananchi wengi kupitia mpango huo.
Msimamizi wa Shughuli za TASAF Tanzania kutoka Benki ya Dunia Bi. Ida Manjoro, akizungumza na waandishi wa habari kufurahishwa na majibu walioyapata kupitia kwa walengwa na mradi huo.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bwana Amedius Kamagenge akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na mafanikio ya Mradi huo kwa shehia hiyo baada ya kupata maelezo kutoka kwa walengwa, na mafanikio waliyoyapata kupitia mradi huo wa Tasaf kunusuru Kaya Masikini Zanzibar.
Meneja wa Fedha wa TASAF Bwana Nyamuko, akizungumza na waandishi wa habari jinsi mfuko huo unavyo wanufaisha wananchi .
Wajumbe wa Nchi Wafadhili wa Mfuko TASAF wakitembelea Kaya masikini katika shehia hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano wao na walengwa
Msimamizi wa Shughuli za TASAF Tanzania kutoka Benki ya Dunia Bi. Ida Manjoro, akiwa na Maboss wa Benki ya Dunia wakitembelea Kaya Masikini katika Shehia ya Muembemakumbi Zanzibar.