Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JK awaonya walafi wa madaraka

$
0
0
Na Kija Elias, Mwanga
Rais Jakaya Kikwete, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa, walioko ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambao wamekuwa waking’ang’ania madaraka, hali ambayo imekuwa ikileta uhasama, chuki na manung’uniko na wingine kukimbilia kujiunga na vyama vya pinzani.

Alisema hayo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na wakazi wa Mwanga katika sherehe za kumuaga Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya.

“Uongozi ni dhamana lakini wapo viongozi wamekuwa ving’ang’anizi katika kuachia madaraka,  hunung’unika na pale wanapokosa nafasi za uongozi huamua kukihama chama wakidhani kuwa ni suluhisho,”alisema.

Alisema wanapoambiwa wawapishe wengine nao waweze kulisukuma gurudumu hilo, huisema vibaya CCM kuwa haithamini na wakati mwingine wamekuwa wakisusia hata  shughuli za maendeleo pindi wanapoambiwa kuachia madaraka hayo.


“Nawaomba viongozi wenzangu tujifunze kutoka kwa Msuya, ameamua kustaafu shughuli za chama ambazo alikuwa akizifanya na hii ndio heshima kubwa kwa taifa,” alisema.

Katika ziara hiyo, Rais Kikwete aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa madarasa na maabara ya taasisi ya kituo cha kiislamu cha Vuchama na kuwataka viongozi hao kuhakikisha kituo hicho kuzitatua changamoto za vitabu na walimu na ili watoto wanaosoma hapo wapate elimu bora.

Awali akitoa tarifa ya kustaafu shughuli za chama, Msuya alimpongeza Rais Kikwete na serikali yake kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya ambayo alisema itasaidia kuiongoza Tanzania kwa miaka mingi ijayo.

Akitoa pongezi hizo, Msuya alisema matatizo ambayo yanaendelea katika bunge la katiba yasiwakatishe tamaa Watanzania na kamwe wasikubali kurudi nyuma.

Katika hatua nyingine, Msuya aliipongeza serikali ya CCM kwa kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 jambo ambalo limesaidia kuifanya Tanzania kupiga hatua kubwa katika utawala wa kidemokrasia.

Alisema viongozi wa chama hawana budi kuendelea kudumisha demokrasia ndani ya chama hicho na  kuondoa makundi ambayo yameanza kujitokeza.


Msuya  ameamua kustafu shughuli za chama ambazo amezitumikia kwa kipindi cha miaka 33.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>