Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mkuchika: Mauaji ya vikongwe yameiporomosha Tanzania

$
0
0
Na Rose chapewa, Mbeya
MAUAJI ya vikongwe, albino, rushwa na kujichukulia sheria mkononi, ni moja ya mambo yaliyosababisha nafasi ya Tanzaniakatika masuala ya utawala bora kushuka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala Bora, George Mkuchika, alisema hayo wakati akifungua  mkutano wa wa kamati ya ushauri ya mkoa  jijini Mbeya (RCC), na kuseoma tabia ya wananchi kujuchukulia sheria mkononi imechangia kwa kiasi kikubwa Tanzaniakushuka kwenye sualala utawala bora.

Alisema katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Shinyanga, Simiyu Mwanza na Mbeya kumekuwa na mauaji yakiwemo ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Alisema pamoja na mauaji hayo, wananachi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi,  hali ambayo inachangia kwa kiasi kiukubwa  Tanzania kufanya vibaya katika utawala bora na kushika nafasi ya 70 kati ya mataifa 170 yaliyofanyiwa utafiti kuhusu utawala bora.


Aidha Waziri huyo pia alizungumzia Suala la mapambano dhidi ya  rushwa  ambalo alisema   ni miongoni mwa viashiria vya utawala bora vinavyochukuliwa na mataifa mbalimbali duniani.

Akizungumzia rushwa, alisema imesababisha  madhara mengi kwa jamii pamoja na misingi ya utawala bora, na kwamba madhara hayo yanaweza kuhatarisha uhai na usalama wa taifa.

Waziri Mkuchika alizitaja athari zitokanazo na rushwa  kuwa ni pamoja na kutotimiza utekelezaji wa majukumu ya serikali, kukwamisha utoaji wa haki na kuongezeka kwa maovu katika jamii.


Madhara mengine ni wananachi kukosa imani na serikali yao na kujichukulia sheria mkononi, kukosekana huduma muhimu za kijamii, kutolewa huduma duni, kuwa na viongozi wasio waadilifu, kusababisha kupungua kwa pato la serikali na hivyo kupunguza uwezo wa serikali katika kuhudumia wananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>