MWALIMU mkuu wa skuli ya sekondari ya Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Hamad, akiwaonyesha wajumbe wa Jumuia ya watu wa Kengeja ‘KEDO’ waishio Dar –es Salaam, msingi wa jengo la madarsa , mara baada ya ujumbe huo kukabidhi vifaa kadhaa kwa skuli hiyo (picha na Haji Nassor, Pemba)
WAISLAMU wa kijiji cha Kambini kichokochwe wilaya ya wete Pemba, wakiwa katika kazi za usafi wa kung’oa majani kwenye jengo lao jipya la msikiti, mbalo wanalijenga kwa nguvu zao, huku msaada ukihitajika ili wahamie (picha na Haji Nassor, Pemba)
KATIBU wa Jumuia ya Mazingira ya shehia ya Kambini Kichokochwe ‘JUMAKA’ wilaya ya wete Pemba, nd: Bakar Suleiman Juma, akigagua kitalu chao cha miche 5,000 ya mikarafuu, ambapo wiki ijayo wanatarajiwa kuwauzia wananchi na serikali (picha na Haji Nassor,
HALI ya majengo ya afisi za askari wa magereza eneo la Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, imekuwa ya kusikitisha kutokana na kuchakaa kwa muda mrefu, na kuwapa hofu askari hao, ambapo kwenye jengo hili wakizungumza na watendaji wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)