Mkufunzi wa mafunzo ya utoaji huduma bora kwa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bwa. Peter Ssali kutoka Uganda akifundisha katika mafunzo hayo
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakimskiliza kwa makini Mkufunzi wa Peter Ssali (hayupo pichani) katika mafunzo yasiku tatu juu ya utoaji huduma bora kwa Bodi hiyo ili kuwa sambamba na Bodi za vyakula za Afrika Mashari.
Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji akitoa tarifa kwa wandishi wa Habari juu ya kupatika kwa wagojwa watatu wa Homa mbaya ya (DENGUE) Visiwani hapa, na kuwataka wananchi kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuangamiza mazalio ya Mbu, kufyeka vichaka vilivyo karibu na makazi namengineyo ili kujinginga na kutafunwa na Mbu huyo.
Mkuu wa kitengo cha kudhuia na kudhibiti maradhi Zanzibar Dkt. Salma Masauni akitoa ufafanuzi kuhusiana na ugonjwa wa Dengue uliojitokeza Nchini Tanzania na zaidi ya Wananchi 400 wamelazwa katika hospitali za Dar-es-Salaam, alipokuwa akizunguza na Waandishi wa habari kuhusiana na ungonjwa huo. (kulia) Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji.
Baadhi ya wandishi wakisikiliza kwa makini tarifa hiyo.Mkufunzi wa mafunzo ya utoaji huduma bora kwa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bwa. Peter Ssali kutoka Uganda akifundisha katika mafunzo hayo