Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

NMB watakiwa kufikisha huduma vijijini

$
0
0
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Uongozi wa Benki ya NMB una wajibu wa kufanya utafiti wa kina katika muelekeo wa kuongeza Matawi yake katika sehemu tofauti nchini wakilenga zaidi maeneo ya Vijijini ili kuwapa fursa Wananachi walio wengi wa maeneo hayo kupata huduma za kifedha.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo mara baada ya futari  ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo na kuhudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo wateja wa benki hiyo futari ambayo ilifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Migombani Mjini Zanzibar.
 
Balozi Seif alisema hivi sasa vipo Vijiji vingi vya kisasa ndani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinahitaji kupatiwa huduma za Kibenki jambo ambalo endapo watapatiwa Matawi ya Benki linaweza kuwaondoshea usumbufu wa msongamano wanaoupata wakati wanapofuata huduma hizo Mjini.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akivitolea mfano baadhi ya Vijiji hivyo kuwa ni pamoja na Nungwi, Kiwengwa na ukanda wa Mkoa wa Kusini Unguja maeneo ambayo hivi sasa yamesheheni Hoteli kadhaa ya Kitalii zinayohitaji huduma hizo.
 
Aliupongeza Uongozi na Wafanyakazi wa Benki ya NMB kwa kusaidia huduma na kufanya kazi kubwa ya kutatua kero za Jamii kitendo ambacho kimesababisha Benki hiyo kupendwa na Wananchi kwa vile bado inaendelea kutoa huduma zaidi vijijini.

Aliwaomba Wananchi kujiunga na NMB kutokana na huduma inazotoa Benki hiyo katika kipindi kifupi tokea kuanzishwa kwake na kufikia hatua ya kuungwa mkono hata na Serikali kutokana na mfumo wake wa kufika katika maeneo ya Wananchi wa kawaida.
 
“ NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia vikalio katika Maskuli mbali mbali hapa Zanzibar. Ukweli ni moja kati ya Benki zinazopendwa hapa Zanzibar. Hata ile mikopo ya JK na AK iliyoandaliwa kuwafikiwa wananachi ili kupunguza umaskini pia ilipitishwa katika Benki hiyo ya NMB “. Alisisitiza Balozi Seif.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi wa NMB kufanya kazi ya ziada katika kuhakikisha misururu ya wateja wao hasa wale watumishi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wanaochukulia mishahara yao katika Benki hiyo inaondoka.
 
“ Unafikia hatua ya kuwaonea huruma wateja wa Benki yenu hasa ndugu zetu wa JWTZ, Polisi na Taasisi nyengine za Muungano wanaochukulia mishahara yao wanalazimika kupanga misururu mirefu ya kusubiri mishahara yao na kujikuta wakipoteza muda mrefu “. Akafafanua Balozi Seif.
 
Mapema Meneja wa Benki ya NMB Abdulmajid Mussa Nsekela alisema katika kukabiliana na usumbufu unaowapata wateja wao Uongozi wa Benki hiyo  umejikita kuongeza Tawi jengine la NMB Mwezi ujao katika eneo la Mwanakwerekwe pamoja na huduma za ATM Tano katika Maeneo ya Vikosi ya Jeshini na Ziwani.
 
Abdumajid Mussa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza msongamano uliopo  wa wateja wao hatua ambayo pia itakwenda sambamba na huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu za mkononi mara baada ya kukamilika kwa mawasiliano kati ya Uongozi wa Benki hiyo na Makampuni ya Simu.
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>