Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wakimbizi wanapaswa kusaidiwa, jamii yatahadharishwa

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
JAMII nchini imetakiwa kutambua kuwa wakimbizi na wahamiaji wasio rasmi, wana haki ya kuhudumiwa, kusikilizwa na kusimamiwa kama walivyo binadamu wengine.

Mbali na hilo pia wanatakiwa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kuwa na vibali vya kuingia nchi nyingine.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Mafunzo kwa Vitendo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), anayehusika na Usalama , Nicholas Gichubiri ,wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari mkoa wa Dodoma iliyohusu masuala ya wakimbizi na wahamiaji iliyoandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji(IOM).

Alisema jamii inapaswa kupewa elimu juu ya sheria za mipaka ya nchi ili kuzuia mkanganyiko unaoweza kujitokeza baina ya nchi na nchi ama wananchi husika ikiwa ni pamoja na kutafuta njia nzuri itakayosaidia kutohalalisha kundi hilokuingia nchini.


Kwa upande wake , Ofisa miradi taifa, Charles Mkude, aliwaasa waandishi wa habari kufanya uchunguzi wa kina juu ya habari wanazozitoa kuhusiana na masuala ya wakimbizi na wahamiaji wasio rasmi ili kuepuka kuwa midomo ya kusemea watu.

Alisema ni vyema wanahabari wakajiuliza maswali ya ziada kwa kile wanachoambiwa juu ya wakimbizi ama wahamiaji wanaoingia nchini ikiwa ni pamoja na kujua sababu za wao kuingia nchini kabla ya kuandika habari zao ili kuleta maana kamili ya habari hiyo.



Aidha aliwataka kuwa na uelewa wa kutosha wa lugha za kimataifa hasa kiingereza ili kuleta urahisi katika utendaji wa kazi zao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>