Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Viwavi jeshi vyaathiri mavuno ya mpunga kaskazini Unguja

$
0
0
Na Husna Mohammed
WAKULIMA wa mpunga mkoa wa kaskazini Unguja, wamesema msimu wa mavuno ya mpunga kwa mwaka huu ni mabaya ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wakulima hao walisema sababu kubwa ya mavuno ya zao hilo kuwa mabaya ni mashamba yao kuvamiwa na viwavi jeshi pamoja na kunguni mgumba.

Pandu Mtumwa na Mwajuma Kombo wa kijiji cha Kinyasini, ambao wanalima katika bonde la Kibokwa, walisema pamoja na uvamizi wa wadudu hao, pia Idara husika ilichelewa kuwapa dawa za kuuliwa wadudu.

“Mabwana na mabibi shamba walikuja lakini walisema kuwa kama watapeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi watachelewa lakini pia walisema wadudu hao ni wagumu wa kufa,” walisema.

Hata hivyo, walisema wako baadhi ya wakulima walipata kunyunyuziwa dawa huku tayari viwavi hivyo vilikwishaleta athari kubwa ya zao hilo.

Aidha Mwandiwe Makame Ali, mkaazi wa Chaani kubwa, alisema  mpunga karibu ekari moja aliyolima umevamiwa na viwavi jeshi.
“Mpunga wangu ulikuwa mzuri sana lakini ulipovamiwa na viwavi jeshi ulikufa mwingi na mchache uliochipua hakuzaa vyema,” alisema.

Nae Mwandiwe Makame Ali wa kijiji cha Chaani kubwa, alisema yeye ni miongoni mwa wakulima wa mpunga walioathiriwa viwavi jeshi katika konde yake.

“Kwa kawaida nalima nusu ekari na kuvuna vipolo hadi 15 lakini kwa mwaka huu naona mavuno yatakuwa mabaya sana kwani hata nikipata basi itakuwa polo nne  hadi tano,” alisema.


Akizungumzia kuhusu dawa za kuulia wadudu, alisema licha ya kufika bibi shamba lakini hakuna huduma iliyotolewa ya kuua wadudu hao.

“Bibi shamba ni hodari kwani anatutembelea mara kwa mara lakini hakuna msaada tuliopata kwa ajili ya kuulia wadudu hawa na ndio maana wakatuathiri sana,” alisema.

Kwa upande wake, mkaazi wa kijiji cha Mkokotoni, Hadia Makame, anaelima bonde la  Fungu refu, alisema eneo hilo halikuathiriwa na viwavi jeshi lakini aliomba Idara husika kuwapatia mbegu na mapema na dawa ya kuulia wadudu na magugu wakati muafaka.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ ,Riziki Simai, akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Gamba, alikiri wakulima kuvamiwa kwa viwavi jeshi na kunguni mgumba .

“Kwa kweli msaada wa serikali kwa mwaka huu haukuwa mzuri kwani wakulima wengi mpunga wao uliathiriwa na wadudu na kwa wakati uliobaki hawakuwa na mbegu wala mbolea  na kusababisha wengine hawakupanda tena mpunga,” alisema.

Aliyataja mabonde yaliyoahiriwa na wadudu hao kuwa ni pamoja na bonde la Mvivu, Kilombero, Kibokwa, Upenja , Pangeni na mto wa maji.

Mapema Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar, Mtumwa Kheir Mbarak, aliliambia baraza la wawakilishi kwamba viwavi jeshi vilivamia mashamba mengi ya mpunga hasa Unguja.
Alisema karibu eka ri 400 za mpunga wilaya ya Kati na Kaskazini ‘A’ zimevamiwa na wadudu hao.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>