Na Hafsa Golo
MBUNGE wa jimbo la Kwahani, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Zanzibar inakusudia kupeleka mswada bungeni kudai maslai yake kama mjadala kuhusu katiba mpya utashindikana kuendelea.
Awamu ya pili ya mjadala kuhusu katiba mpya unatarajiwa kuanza Agosti 5.
Dk. Mwinyi ambae ni Waziri wa Ulinzi, alisema hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya jimbo la Kwahani.
Alisema mswada huo utazingatia suala la uchumi na maslahi ya Zanzibar ambapo mambo mbali mbali ya msingi yatawasilishwa, ikiwemo suala la mafuta na gesi.
Alisema mswada huo huenda ukapelekwa katika bunge la kawaida mwezi Novemba, lakini iwapo katika mpya itashindikana.
Juzi Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Khamis Hamad, alisema mjadala wa katiba hautawezekana kuendelea bila ya kuwepo wa jumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao wanasusia mjadala huo.
Alisema hakuna sababu ya msingi ya kukosekana maslahi ya Zanzibar hasa hata kama katiba ya sasa itaendelea ikizingatiwa bunge ndio chombo kikuu cha maamuzi ya sheria za nchi.
"Naamini Zanzibar itakuwa na maslahi mazuri sina wasiwasi hata kama bunge la katiba halikukaa,"alisema.
Akizungumzia suala la kugombea uongozi alisema hajawa na maamuzi hasa akizingati bado ni mapema.