Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanaodaiwa na ZSTC wahimizwa kulipa

$
0
0
Na Masanja Mabula,Pemba
WAKULIMA wa karafuu waliokopeshwa fedha na Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)  katika wilaya ya Wete huenda wasipate mikopo ya fedha  kwa msimu huu  iwapo watashindwa kurejesha mikopo hiyo waliyokopeshwa msimu uliopita.

Akizungumza na masheha wa wilaya hiyo  ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman, alisema shirika la ZSTC linadai shilingi milioni 23 kutoka kwa wakulima wa karafuu wa wilaya hiyo fedha ambazo walikopeshwa msimu uliopita.

Alisema katika msimu uliopita shirika lilikopesha wakulima wa karafuu katika wilaya hiyo zaidi ya shilingi milioni 138 ambapo fedha ambazo hadi sasa zimerejeshwa ni shilingi milioni 115.12.

Aliwataka Masheha kuzifuatlia fedha hizo kwa wakulima waliokopeshwa na kuwahimiza kurejesha fedha hizo ili kuliwezesha shirikia kuendesha shughuli zake za kuwahudumia wakulima kwa ufanisi zaidi.


Aidha alisema serikali ya wilaya hiyo inakusudia kuwaita wadaiwa ambao wameshindwa kurejesha mikopo ambapo hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza na iwapo wataendelea kukaidi  watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine aliwataka masheha kuwa waadilifu katika kusimimia suala la ujazaji wa fomu kwa wananchi watakao hitaji kukopeshwa na shirikia katika msimu huu wa mavuno.


Nao baadhi ya masheha waliahidi kusimamia uadilifu ili kuona zoezi la ukopaji wa fedha linafanikiwa na wanaokopeshwa ni wale ambao wana uwezo wa kurejesha kwa wakati.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>