Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wenye ulemavu waomba wakalimani

$
0
0
Mwanrafia Kombo na Amina Masoud, MCC
JUMUIYA ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) umeiomba serikali kufanya jitihada za makusudi za kuwasomesha wakalimani kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wao.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Rashid Ali Mohamed,ofisini kwake Kikwajuni, wakati akizungumza na waandishi wa hari hizi.
Alisema kuwepo kwa wakalimani kutawasaidia watu wenye ulemavu kufuatilia matukio mbali mbali yanayotokea katika jamii.
Alisema lengo la kuanziwa jumuiya hiyo ni kuwakusanya pamoja watu wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuwapatia fursa mbali mbali ikiwemo elimu na mikopo.
Alisema fursa nyengine ni kupatiwa misaada kutoka jumuiya ya wafanyakazi wa kujitolea (VSO) ambapo makao makuu yake yapo nchini Uingereza katika masula ya kilimo cha mboga mboga.

Pamoja na hayo pia wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mitazamo finyu ya jamii juu ya kundi hilo na kuwapa majina mabaya ambayo hayafai kuitwa binadamu.
Aidha alisema watu wenye ulemavu hawapati haki katika vyombo vya sheria na kusababisha kesi nyingi zinazowahusu kufutwa.
Aliviomba vyombo vya shieria kubadilisha vipengele vya sheria ambazo zinawabana walemavu na kuzingatia haki zao katika sheria ya ushahidi. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>