Na Tatu Makame
JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, linafanya operesheni ya kukabiliana na wezi wa mazao katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kamanda wa Polisi mkoa huo, Mkadam Khamis Mkadam, , alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake Madema.
Alisema lengo la opereshen hiyo ni kuzuia wizi wa mazao ambao huongezeka zaidi katika kipindi kama hiki.
Alisema mazazo kama ndizi,muhogo,majimbi,viazi vikuu ndivyo vinavyoibiwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika kipindi cha Ramadhani, hivyo jeshi la polisi linataka kukomesha wizi huo.
Alisema operesheni hizo zinafanywa katika barabara kuu zinazotumiwa na gari za shamba kupeleka mazao masokonini.
Maeneo ambayo operesheni hiyo itafanywa ni Fuoni, Mwera na barabara nyengine zinazotumiwa kuingiza mazao mijini.