Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

6.189 b/- kutengeneza barabara Unguja,Pemba

$
0
0
Na Salum Vuai, Maelezo
SHILINGI bilioni 6.189, zitatumika kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo barabara mbali mbali Unguja na Pemba.

Taarifa kutoka Mfuko wa Barabara zimefafanua kuwa shilingi bilioni 3.278 zitagharamia barabara za Unguja, na wakati zile za Pemba zitatumia shilingi bilioni 2.264.

Aidha shilingi milioni 647 zimetengwa na mfuko huo kwa ajili ya kazi za dharura, matengenezo ya vifaa na mchango kwenye miradi ya serikali, ambapo pia kwa mwaka huu kazi zenye thamani ya ya shilingi bilioni 3.281 sawa na asilimia 53 ya fedha zote zitafanywa na wakandarasi binafsi. 

Hafla ya utiaji saini mkataba wa kutekeleza kazi hizo, imefanyika jana ambapo Mfuko wa Barabara uliwakilishwa wa Mwenyekiti wa Bodi, Ali Abdalla Suleiman na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Dk. Juma Malik Akili alisaini kwa niaba ya wizara yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Mfuko huo, makubaliano hayo ya kazi yanafanyika kukidhi mahitaji ya sheria mfuko kifungu 8 A (b) inayoiruhusu bodi kuingia mkataba wa kazi na Wizara inayoshughulika na barabara au wakala mwengine anaekubalika.


Utekelezaji wa kazi hizo unafanyika baada ya kukamilika kwa mpango kazi wa matengenezo hayo kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaoanzia Julai 2014 hadi Juni mwaka 2015.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Mfuko huo imesema mpango wa mwaka huu wa matengenezo umezingatia zaidi kuhami barabara kubwa, madaraja na huduma za usalama wa barabara.

Barabara zitakazonufaika na mpango huo kwa upande wa Unguja ni, Mwanakwerekwe Makaburini/Fuoni, Bumbwini/Kiongwe skuli, Magereza/Kwa Mchina/Tomondo na Michenzani/Mtendeni.

Nyengine ni Mshelishelini/Gamba, Amani/Mtoni na daraja la Kitope, alama za barabarani na taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara ya Malindi.    

Kwa upande wa Pemba ni Ole/Konde, Kangani/Mkanyageni, Chake Chake/Mkoani, katika eneo la Kwachangawe, Pandani/Mlindo na barabara nyenginezo.

Bodi ya Mfuko wa Barabara imehakikisha kuwa wakati wote wa kazi hizo, wataalamu wa kiufundi na fedha watafanya uangalizi wa karibu kuhakikisha ufanisi wa kazi hizo.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mwishoni mwa mwaka, Mfuko wa Barabara utaajiri wakaguzi huru wa fedha na kazi kwa ajili ya kupata maoni yanayohusu namna fedha hizo zitavyotumika. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>