Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tume ya Warioba yaombwa kuwanasihi UKAWA kurudi bungeni

$
0
0
Na Rose Masaka, Maelezo
BALOZI wa amani nchini Tanzania, Risasi Mwaulanga, ameiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuwashawishi wajumbe wa bunge la katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurudi bungeni, kwa sababu tume hiyo ina ushawishi mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Balozi huyo pia aliwanasihi viongozi wa dini na asasi za kiraia kutochoka kuwashawishi UKAWA kurudi bungeni kuhakikisha Watanzania wanapata katiba waitakayo na sio katiba ya kisiasa.

Aidha alisema kauli za vitisho na uvunjifu wa amani vinapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.

Aliwaomba UKAWA kukubali maoni ya Watanzania walio wengi ya kuheshimu fedha za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za nguvu  hazitapingwa.

 “Nawaomba UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyomnaliza  changamoto za Watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale,” alisema.

Alisema  ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo Watanzania tunapaswa kutambua ni katiba gani  wanayoitaka na kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora.

Wakati huo huo, Fatina Mathias kutoka Dodoma, anaripoti kwamba vyombo vya  ulinzi na usalama vimeombwa  kufuatilia nyendo za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka UKAWA ili kujua nani yupo nyuma yao.

Kauli hiyo ilitolewa na Msemaji wa UVCCM, Paul Makonda, ambaye pia ni mjumbe wa bunge hiloalipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Alisema vyombo hivyo vinapaswa kulichunguza kundi hilo ili kujua nani yuko nyuma yao kutokana na wajumbe hao kuwa na kiburi kilichopindukia.Alitoa wito kwa Watanzania na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa amani, umoja na uhai wa wananchi upo mikononi mwao na nia  ya UKAWA sio nzuri kwa mustakabali wa taifa.

“Rais hawezi kutekeleza madai ya UKAWA ya kulivunja bunge maalum la katiba kwa kuwa hawezi kuwa sehemu ya kuvunja sheria,kwa nini UKAWA wanataka kumlazimisha Rais avunje sheria  wakati hana mamlaka hayo kisheria zaidi ya mamlaka ya kuteua wajumbe wa kundi la 201,” alisema.

Alisema mchakato wa kisheria lazima uende kisheria na kuwataka wananchi kutowaunga mkono kwa uamuzi wao wa kulisusia bunge hilo kwa kuwa kufanyqa hivyo ni kushiriki kuvunja sheria.


Alisema kinachoshangaza kutoka kwa UKAWA ni kubadilisha madai yaokila kukicha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>