Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JK:Uraia pacha muhimu.Ikulu yasema Rais hana ubavu kulivunja bunge

$
0
0
Na Fatma Kitima, Dar es Salaam
WAKATI msuguano kuhusu uraia pacha ukiendelea katika bunge maalum la katika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amesema suala hilo ni muhimu lakini serikali haina mamlaka ya kulazimisha.

Hata hivyo, alisema suala hilo limewekwa ndani ya rasimu ya  katiba mpya kukujadiliwa.

Lakini kutokana na umhimu huo ,Serikali ya Muungano na Zanzibarzitaendelea kutoa ushirikiano na kulishughulikia kwa umakini zaidi ili kuondoa changamoto zilizopo.

Rais Kikwete alisema hayo jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili, uliowakutanisha wanadiaspora wanaoishi ndani na nje ya nchi wenye lengo la kujadili na kubadilishana mawazo pamoja na kuangalia changamoto zinazowakabili huko ughaibuni.

Aidha alitoa wito kwa Watanzania wanaoishi  nje ya nchi,kutumia fursa walizonazo kuwekeza na kuwashawishi wawekezaji wa kigeni kuja Tanzania ili kukuza uchumi wa taifa.

Aliwakumbusha kuthamini nchi yao na kuzisaidia familia zao kwa kuzitembelea mara kwa mara badala ya kuishia mijini wakati wanapofika nchini Tanzania na kutojua mazingira na utamaduni wa kwao hali inayodhihirisha kwamba wamezitenga familia zao.

Alisisitiza kutoa msaada wa kuwaendeleza ndugu zao kielimu ili kujikwamua na umaskini na baadae familia ziwe mabalozi wa kueneza elimu na chachu ya maendeleo kiuchumi.


“Natoa wito kwa wanadiaspora wote mtumie fursa hii na uelewa wenu kuwashawishi watu na makampuni yenye uwezo na nguvu ya kuwekeza hapa nchini kwani hakuna nchi yeyote inayokua kiuchumi bila uwekezaji wa ndani au nje nchi,” alisema.

Kwa upande wa washiriki wa mkutano huo, walitoa ahadi kwa serikali kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha na kuangalia maeneo ya uwekezaji ndani ya nchi kwa kuwashawishi wawekezaji kuwekeza nchini ili kupanua uchumi  na kupunguza umaskini.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisema katiba haimruhusu Rais kulivunja au kuliahirisha bunge la katiba.

 Alisema wapinzani lazima waende kusoma tena sheria ya mabadiliko ya katiba kwa undani na watajiridhisha kuwa Rais hana ubavu wowote kisheria kuahirisha wala kulivunja bunge la katiba linaloendelea sasa.

Aliwataka pia wapinzani kama wana hoja yoyote kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ili kusaidia upatikanaji wa katiba mpya lakini wasitarajie kusimamishwa kwa mchakato kwani ni kinyume cha sheria.


 Kuhusu maandamano, alsiema hayatakuwa na msaada wowote kupata katiba mpya zaidi ya kuleta vurugu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>