Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hospitali ya Kivunge yaomba usafiri

$
0
0
Na Fatma Kassim, Maelezo
HOSPITALI ya Kivunge iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja inakabiliwa na tatizo la usafiri wa wajawazito na wagonjwa wengine wanaohitaji huduma hiyo.

Wanaoathiriwa zaidi na tatizo hilo ni wale wanaopewa rufaa ya kwenda Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kwa matibabu zaidi.

Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge, Dk. Shau Ali Hamdan alisema  hospitali hiyo ina gari moja tu la kubebea wagonjwa ambalo hata hivyo linatumiwa kwa shughuli nyengine za kiofisi.

“Ni usmbufu mkubwa kwani linapotakiwa kubeba wagonjwa linakuwa katika shughuli zingine za ofisi na linapotakiwa kwa shughuli za ofisi linakuwa katika shughuli ya kubeba wagonjwa,” alisema na kulitaja gari hilokuwa ni Ambulance.

Alisema pamoja na uwepo wa gari hilo, Dk Hamdan alisema wanakabiliwa na tatizo la mafuta ya kuendeshea gari hilona inapotokezea mgonjwa kupatiwa rufaa, inamlazimu kuchangia  shilingi 30, 000 kwa ajili ya mafuta.

Alisema Wizara ya Afya imepanga kuwapatia lita  400 za mafuta kila mwezi lakini hupatiwa chini ya kiwango hicho jambo linalokwamisha utekelezaji wa majukumu yao.

Gari hiyo imetolewa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) mwaka 2009 kwa ajili ya kuwahudumia wajawazito wanaopatiwa rufaa kupelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Dk. Hamdan alisema hospitali   ya Kivunge inategemewa na wakaazi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwemo wale wanaotoka mbali kamakisiwa cha Tumbatu, Kijijini Matemwe na sehemu nyengine.


Uwezo wa hospitali hiyo inapokea wastani wa wagonjwa 150 kwa siku, na  wajawazito wanaohudumiwa kila mwezi wastani wa 250 na wanaopewa rufaa ni 22 kwa mwezi.

“Kuna baadhi  ya wajawazito wanakuja moja kwa moja  kujifungua  hapa,  lakini, wengine wanakuwa weshacheleweshwa,  wengine wanakuja  kwa kupatiwa rufaa na  mara nyingi akifika hali ishakuwa mbaya,  inabidi   sisi tumpatie rufaa kwa kumuwahishia Mnazimmoja na  hapo inabidi mgonjwa achangie mafuta”, alifahamisha Dk. Shau.

Wajawazito na wagonjwa wengine wanapopta rufaa kupelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja  wanapokosa usafiri hospitalini huwa wanatumia gari za kukodi ambazo hulazimika kulipia zaidi ya 30,000.

Dk. Hamdan alisema kutokana na hali hiyo, lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi litakuwa gumu kufikiwa iwapo mamlaka husika haitojipanga ipasavyo katika kuzipa kipaumbele huduma za mama wakati wa ujauzito wake, anapojifungua na baada ya kujifungua.

Wastani wa vifo vya wajawazito vinavyotokea kwa kila mwaka ni vinne katika hospitali hiyo.

Mkakati wa Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA), umelenga kupunguza vifo vya uzazi kutoka vifo 473 mwaka 2007 hadi vifo  170 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2015.

Malengo ya Millenia namba tano  ni kupunguza vifo vya uzazi  kutoka 473 mwaka 2007 hadi 170 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo  mwaka 2015.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Mohammed Saleh Jidawi, alisema, nia ya Wizara hiyo ni kutekeleza mikakati ya kuimarisha huduma za wajawazito katika hospitali pamoja na vituo vya afya huku wajawazito wakitakiwa kutochangia  huduma wakati wa kujifungua.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>